ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 2, 2012

MATUKIO YA UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA BADO YAITESA POLISI MWANZA

Siku 18 tangu lilipotokea tukio la mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa mwanza liberatus barlow, usiku wa kuamkia leo majira ya saa 8:00 za usiku katika eneo la Nyegezi watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia makazi ya Wakili wa kujitegemea Elias Hezron na kumpigwa risasi  ya tumbo kisha kumpora kompyuta yake ya mkononi (laptop), simu tatu ikiwemo moja ya mkewe na kutokomea kusikojulikana.

Wakili Elias Hezron wa kampuni ya uwakili ya JURISTIC LAW CHAMBER inayo milikiwa na Hon. Justice Nchalla, Outa & Hezron, Partiner Advocte ya jijini Mwanza ambaye amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ambapo hali yake inadaiwa kuwa mbaya hivyo madaktari wanaendelea kumpatia tiba ili kuokoa maisha yake.

Akizungumza na Clouds kwa njia ya simu kaka wa wakili huyo George Hezron ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa Novemba 2 mwaka huu majira ya usiku baada ya muda mfupi kukatika kwa umeme ambapo wakili huyo akiwa na mkewe walisikia kishindo cha kuvunjwa geti na hatimaye mlango kisha watu wawili wasiotambulika sura zao waliingia ndani  huku wengine wakionekana nje ya nyumba na kumtaka Bw. Elias kuwapatia kompyuta yake ya mkononi, simu zake zote naye kukaidi agizo la watu hao.

"Baada ya kumuamuru na yeye kukataa  kutii kuwapatia kompyuta ndipo mmoja wa watu hao aliamua kumpiga na kitu kizito (nondo) kichwani naye kumkaba mwenzake hali iliyopelekea purukushani na kumzidia nguvu jambazi, ndipo mwenzake alipoamua kutoa silaha na kumfyatulia risasi tumboni kisha kupora vitu walivyohitaji na kumwamuru mke wa wakili huyo pia kuwapatia simu yake ya mkononi na kisha wakatokomea kusikojulikana" Alieleza kwa masikitiko kaka wa wakili huyo.

Bw. George amefafanua kuwa baada ya kupora kompyuta hiyo na simu hizo watu hao walitokomea bila kuchukuwa kitu kingine huku kompyuta iliyochukuliwa ikionekana kuwa na kumbukumbu na nyaraka za kesi mbalimbali ambazo wakili huyo amekuwa akizisimamia kwenye mahakama za mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani hali inayoonyesha kuwa watu hao walikuwa wamekusudia kupora nyaraka hizo.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Bi. Lilian Matola amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina na chanzo cha tukio ikiwa ni pamoja na kuwasaka kwa udi na uvumba watu walio husika. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.