ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 27, 2012

WANAOMPINGA WENJE WAMFANYIA VURUGU WAKATI AKABIDHI MADAWATI, MNYIKA ALIPA AHADI ALIYOITOA MKUTANO WA MWEZI WA 4 KUCHANGIA MADAWATI, MBOWE, ZITO KABWE, HALIMA MDEE, ESTER BULAYA, VICK KAMATA WATAJWA LIST YA WANAO DAIWA. JEH! WALITOA AHADI HEWA KUCHANGIA MADAWATI NYAMAGANA?

Mbunge wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza Ezekiel Wenje akihutubia wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Sahara,  ambapo pia mbunge huyo alitumia fursa ya mkutano huo kukabidhi madawati 400 yaliyotengenezwa kwaajili ya kutatua tatizo la madawati kwa shule za msingi jijini Mwanza. 


Pichani ni baadhi ya madiwani wa CHADEMA kwa  kata mbalimbali jijini Mwanza pamoja na makada wa chama hicho waliohudhuria kusanyiko hilo kwenye uwanja wa Sahara leo jioni hapa jijini Mwanza. 

Mnamo tarehe 7 mwezi 4 mwaka huu chama hicho kiliendesha harambee kwenye uwanja huu wa Sahara hivyo madawati haya ni matokeo ya changizo lililofanyika kwa kishindo kwa wananchi kujitokeza kuchangia hadi shilingi ya mwisho akibani mwao lakini baadhi ya wadau wengi na wengine waheshimiwa wabunge wenye majina waliahidi kwenye mkutano huo wa mwezi wa nne mwaka huu lakini mpaka leo ambapo tunaelekea kuumaliza mwaka 2012 hawajatimiza ahadi zao licha ya kupigiwa simu na kufuatiliwa mara kwa mara... Hakika ni maswali kwa wananchi wa jimbo hili.

  
Jumla ya shilingi milioni 56 ikiwa ni ahadi na pesa taslimu zilipatikana kwenye changizo la madawati lililofanyika mnamo mwezi wa nne 2012 ambapo pesa cash iliyopatikana ni shilingi milioni 24 ahadi ambayo haijalipwa mpaka sasa ni shilingi milioni 32. Kujua wanaodaiwa na viwango vya madeni yao kwa ahadi za madawati bofya play ...




Mbunge wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza Ezekiel Wenje akimtambulisha mbunge wa Ubungo Mh. Peter Mnyika kwa wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Sahara,  ambapo mbunge huyo alitumia fursa ya mkutano huo kukabidhi madawati 400 yaliyo tengenezwa kwa ajili ya kutatua tatizo la madawati kwa shule 30 za msingi jijini Mwanza. 

Karibu na robo ya mwisho wakati Mnyika akielekea kuanza kuhutubia joto la timbwili timbwili la vurugu likatokea mara baada ya watu kadhaa waliosadikika kuwa walikuwa wametumwa na maadui wa Wenje ambao wamo ndani ya chama hicho kufanya vurugu kwenye mkutano huo kwa kurusha mawe kwenye kusanyiko hali ambayo ilisababisha baadhi ya waungwana kusambaratika wakihofia usalama wao.


Ili kujinusuru mmoja wa watu hao ilibidi ajisitiri kwenye jukwaa la kuhutubia...


Mdau akitweta mara baada mvua ya makonde kumwangukia.. 


Huyu mwingine alikuwa akilia kwamba wamemfanyia uonevu kumpiga hata kumuumiza yeye ni mwanachama wa CHADEMA na hajatumwa na mtu. 

"Hapa ndipo angalau kuna usalama.." mwananchi akiwa na majeraha yake...

Hatimaye polisi walifanikiwa kufika eneo la kusanyiko haraka iwezekanavyo na kuwaondoa watu hao ambao walikuwa wakinyemelewa na wananchi wenye hasira kali licha ya kukumbilia kwenye jukwaa la viongozi.

Mbunge wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza Ezekiel Wenje akitoa maelekezo juu ya madawati hayo ambayo yametengenezwa kwa mtindo kuwa kila moja linauwezo wa kuketisha wanafunzi watatu.
Orodha ya shule zitakazo nufaika na mpango huo ni pamoja na Shule ya Lake A na B, Shule ya msingi Nyashana  A, B, na C,  Shule ya msingi Nyakabungo B, Mabatini A, B na C, Shule ya msingi Nyerere, Shule ya msingi Mandela, Ngwandu A, B, C na D, Nyagulugulu, Nyakato, Mahina, Mtakuja, Pamba, Hongera na nyingine ndani ya wilaya hiyo....  
Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika amelirudia neno lake lililompiga out Bungeni la kumtaja Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuwa ni dhaifu. Akisema kwamba hapa hakuna mwongozo wa spika, hakuna utaratibu wananchi wamepiga kura....
Kusikiliza Bofya Play...




Wananchi kusanyikoni.


Mbunge Mnyika akikabidhi kiasi cha shilingi laki moja kwa mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje kutimiza ahadi aliyoahidi kwenye mkutano uliofayika tarehe 7 mwezi wa 4, 2012  kuchangia madawati kwa shule za msingi wilaya ya Nyamagana ambapo nyingi ziko katika hali mbaya kwa wanafunzi wake wengi kuketi chini kwenye vumbi na mawe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.