ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 15, 2012

KAMANDA BARLOW KUAGWA LEO JIJINI MWANZA.

Enzi za uhai wake Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow (kulia) hapa alikuwa akitoa ahadi kuchangia mfuko wa Umoja wa wanawake wajasiliamali ulioanzishwa jijini Mwanza ujulikanao kwa jina la KWEA ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alikuwa ndiye mshereheshaji. 

Mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la Polisi Mwanza, Marehemu Liberatus Barlow utaondoka katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando saa 1:00 asubuhi ya leo na kupelekwa nyumbani alikokuwa akiishi marehemu eneo la Pasiansi jirani na kotaz za Marine Service.

Baada ya kufikishwa kwenye makazi hayo mwili huo utakaa kwa muda wa dakika 30 kisha utapelekwa viwanja vya Michezo Nyamagana ambapo kuanzia saa 2:30 Fursa itatolewa kwa viongozi wa kada mbalimbali na wananchi kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza na mikoa jirani kutoa heshima zao za mwisho kwa mchapakazi huyu aliyeiaga dunia katika mazingira ya kutatanisha.
  
Baada ya zoezi hilo kukamilika kwa nafasi yake mwili wa marehemu Kamanda Liberatus Barlow utaondolewa kwa msafara hadi Airport Mwanza ambapo utasafirishwa kwenda nyumba ya marehemu jijini Dar es salaam ambako familia yake inaishi.

Kesho (jumanne)  zitafanyika lojistics mbalimbali ikiwa ni pamoja na  Maofisa wengine wa jeshi la polisi Makao makuu (jijini Dar es salaam),  wananchi, majirani na marafiki kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kamanda Barlow, kisha mwili utasafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro hatimaye Marangu kijijini kwao kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya jumatano.

Kwa hivi sasa viongozi mbalimbali wamekwisha wasili jijini hapa kwaajili ya taratibu za leo tangu juzi tunaye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Emmanuel Nchimbi, tunaye pia mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI Robert Manumba na timu yake, viongozi wengine ambao walikuwa kwenye mbio za mwenge wa Uhuru mkoani Shinyanga Mh. Asha Rose Migiro na wengine wengi. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.