ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 13, 2012

BREAKING NEWS YA USIKU HUU: KAMANDA WA POLISI MWANZA AUAWA

Marehemu Kamanda Liberetus Barlow (kulia) enzi za uhai wake akizungumza na vyombo vya habari jijini Mwanza. 

Ilikuwa ni majira ya saa  8 usiku huu napata taarifa ambazo hatimaye zinathibitishwa kutoka kwa waugwana kuwa  Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow amefariki dunia kwa kupigwa risasi usiku huu maeneo ya hotel Tai 5, Kitangili jijini Mwanza .


Marehemu Kamanda Liberatus Barlow alifariki kabla ya kufikishwa katika hospitali ya Bugando ambapo inadaiwa alivamiwa na watu takribani wanne waliokuwa wamevalia mavazi ya polisi jamii ndipo aliposimamishwa na baada ya kusimama watu hao walimmiminia risasi kufuani na kusababisha  kifo chake

Imeelezwa kwamba Marehemu Kamanda Liberatus Barlow alikuwa akitoka kwenye harusi na alikuwa na mtu mmoja
  kwenye gari aliyekuwa akimsindikiza mtu huyo ambaye ni mwanamke yeye hakudhurika na chochote katika tukio hilo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.Eng. Evarist Ndikilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza ameshathibitisha kutokea kwa tukio hilo la kifo cha kamanda Liberatus Barlow.

Aidha taarifa zaidi kuhusu tukio hilo tutaendelea kuwajuza kwa kadri tutakavyozipata hapa


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.