ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 24, 2012

AIRTEL YAWAZAWADIA 500% BONUS YA MUDA WA MAONGEZI KWA WATEJA WAKE.


Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor akiongea  na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya “Jipatie Mara 5” inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya  wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku  . Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco. Kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Cheikh Saar.

Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor akiongea  wakati wa uzinduzi wa promosheni ya “Jipatie Mara 5” inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku ikiwa ni sawa na 500% bonus ya muda wa maongezi. Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco.
Mkurugenzi wa Masoko Cheikh Saar akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa promosheni ya “Jipatie Mara 5” inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku. Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco. katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya


Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor (katikati) pamoja Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano Mallya (kushoto)  na Mkurugenzi wa Masoko Cheikh Saar (kulia) kwa pamoja  wakionyesha moja ya vipeperushi vya promosheni mpya ya “ Jipatie Mara “ wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya inayowawezesha wateja wa Airtel kupata mara tano ya muda wa maongezi kutokana na  wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku. Uzinduzi huo umefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco.
Press Release
Airtel yawazawadia 500% bonus ya Muda wa Maongezi kwa wateja wake
·         Wateja wa Airtel kupata mara tano ya muda wa maongezi
·         Hakuna haja ya kujiunga  kwenye “ Jipatie Mara 5”
Dar es salaam Octoba 2012 Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel leo imezindua promosheni mpya kabambe itakayowazawadia wateja wake nchi nzima. Promosheni hii ijulikanayo kama “Jipatie Mara 5” itawawezesha wateja wa Airtel kupata MARA TANO  ya wastani wa matumizi ya kupiga simu kwa siku nzima.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangalloor alisema” Airtel tunayofuraha kuwazawadia wateja wetu nchi nzima mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku promosheni hii ya “Jipatie Mara 5”.  Promosheni hii itawazawadia wateja wa Airtel mara 5 ya matumizi yao kama bonus ya muda wa maongezi itakayowawezesha kupiga simu kwenda namba yoyote ya Airtel kwa siku hiyo , hii ni sawa na asilimia 500 ya bonus.

”Tumefanya hivi ili kuendelea kuboresha huduma zetu na pia kuendeleza kudhibitisha dhamira yetu ya  kuwapatia wateja wetu nchini nzima uhuru wa kuongea  aliongeza Elangalloor .”

Akifafanua juu ya promosheni hiyo Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Airtel Beatrice Singano Mallya alisema” kila mteja wa Airtel tayari ameshaunganishwa katika promosheni hii, kinachotakiwa kufanya ni kupiga simu upate bure salio mara 5 ya wastani wa matumizi yako ya siku kadri mteja anavyotumia simu yake kwa kupiga simu ndivyo anajipatia  nafasi  zaidi ya kuzawadia asilimia 500 ya bonus ya muda wa maongezi

“Jipatie Mara 5” ni promosheni kwa ajili ya wateja wa malipo ya awali, kila mteja atapata ujumbe utakaomjulisha wastani wake kwa siku na kisha kupokea ujumbe mara atakapopokea asilimia 500% kutoka Airtel. Kwa maelezo zaidi juu ya  huduma hii piga 0783001001 bure na kuunganishwa moja kwa moja na taarifa mbalimbali za huduma zetu”aliongeza Mallya.

Airtel inaendelea kuboresha huduma za mawasiliano nchini.  kwa kupitia huduma ya Airtel money, Airtel imewawezesha watanzania kupata  huduma za kifedha kirahisi  katika maeneo mbalimbali nchini. Kwa kuthibitisha uwezeshaji wa upatikanaji wa huduma za kifedha Airtel imewawezesha wateja wake kutuma na kupokea pesa chini ya shilling 100,000/= bure bila makato yoyote. Vile vile Airtel imeendelea kupanua zaidi  huduma za internet kwa  kuwezesha miji zaidi ya 30 nchini kupata internet yenye  kasi ya  3.75G .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.