ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 25, 2012

UMOJA WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA MKOA WA MWANZA WAGOMEA SENSA.


Makamu Mweneyekiti wa Umoja wa Wenyeviti wa serikali za mitaa mkoa wa Mwanza Hamza Yusuph Shido akitoa tamko la Umoja huo kutoshiriki SENSA ya watu na makazi, pembeni yake ni Mwita Marwa Meteti ambaye ni katibu mkuu wa umoja huo.
Sikiliza tamko lao kwa ufupi. (Bofya play)
Makamu Mweneyekiti wa Umoja wa Wenyeviti wa serikali za mitaa mkoa wa Mwanza Hamza Yusuph Shido (katikati) akitoa tamko la Umoja huo kutoshiriki SENSA ya watu na makazi, kulia ni Mwita Marwa Meteti ambaye ni katibu mkuu wa umoja huo na kushoto ni naibu katibu wa umoja huo Kipara Mc, Mlemela, Tamko hilo limetolewa ndani ya ukumbi wa ofisi za MPC jana jioni.
BAADHI YA MALALAMIKO YAO.
-Wakanusha makarani wa SENSA kutokea mitaa yao: wengi hawawafahamu.
-Wadai kuwa vijana hawakuchaguliwa badala yake waliopewa ni ndugu za wafanya mchujo.
-Wameamua kususia zoezi la kusimamia SENSA kwani wanafanyishwa kazi katika mazingira magumu hawalipwi posho, wametelekezwa, walaumu kutohusishwa katika uwezeshwaji tokea awali kwenye michakato.
Walioketi mezani mbele ni sehemu ya Wanaumoja wa Wenyeviti wa serikali za mitaa mkoa wa Mwanza waliohudhuria mkutano huo wa kutoa tamko mbele ya waandishi wa habari.

Sehemu ya kusanyiko hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.