ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 11, 2012

MEXICO YAIBANJUA BRAZIL

Timu ya kandanda ya Mexico imewashangaza mashabiki wa mchezo huo kwa kuichapa Brazil kwenye fainali ya Kombe la Olimpiki katika uwanja wa Wembley mjini London.
Oribe Peralta aliipatia Mexico bao la kwanza ikiwa ni sekunde 29 baada ya kipenga cha kuanza mchuano kupulizwa.

Peralta litumia fursa iliyotokana na kosa la beki wa Brazil kuchezea katika nusu ya uwanja kwa upande wa Brail na kuikandika Brazil bao la haraka lililozipeleka pande hizi hadi mapumziko kwa hesabu ya 1-0 kwa Mexico.

Bao la Peralta...
Hili ni bao la kwanza kufungwa haraka zaidi katika kipindi cha miaka 36 ya mashindano ya soka ya Olimpiki. Mshambuliaji huyo huyo alirudi kutikisa nyavu za Brazil mnamo dakika ya 75 kwa mpira wa kichwa.

 Brazil ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia mshambuliaji Givaldino Hulk zikisalia dakika kama tatu hivi kufikia mwisho wa mechi lakini Mexico ikashikilia mabao yake mawili hadi kipenga cha mwisho.

Machungu ya Neymar...
Kabla ya mechi hii, watangazaji wa idhaa ya kiswahili walitabiri ushindi wa Brazil, lakini Mexico ilikuwa na mipango tofauti na fikra za wengi.

Hivyo basi historia inabaki pale pale kwa Brazil kuondoka mashindano haya ya Olimpiki bila medali ya dhahabu ingawa itaondoka na fedha. Jumla ya watu 86,162 wameshuhudia pambano hili ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kuhudhuria mechi yoyote kwenye mashindano haya ya Olimpiki ya London 2012. Jumla ya watu milioni 2,186,930 wamehudhuria mashindano ya mpira ya wanawake na wanaume kwenye Olimpiki hizi.
Maandishi kwa hisani ya bbc Swahili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.