ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 14, 2012

ALLIANCE ACADEMY WAREJEA NYUMBANI NA VIKOMBE VYA USHINDI

Timu za soka za U-14 na U-17 toka Shule ya Alliance Academy ya jijini Mwanza zimeibuka mabingwa katika Mashindano ya Future Stars Rafiki Cup yaliyoandaliwa na Shule ya English Medium ya Future Stars Academy ya mjini Arusha na kushirikisha timu mbalimbali nchini.

Alliance Academy imefanikiwa kuibuka mabingwa kwa michuano hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki na sasa timu zake zimekwisha wasili jijini Mwanza kwaajili ya kujumuika na wadau wake kwa sherehe.

Kaptein wa U17 akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nyumbani jijini Mwanza .
Ambapo timu hiyo ilishinda michezo yake yote mitatu bila kupoteza.

Kaptein wa U14 akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nyumbani jijini Mwanza .
Ambapo timu hiyo imekuwa mshindi wa kwanza mara baada ya kucheza michezo mitatu ikishinda miwili na kutoka sare mchezo mmoja na katika ushindi huo haikufungwa hata goli moja, magoli matano ya kufunga na pointi 7.

Furgency Novatus ni kocha wa timu za soka shuleni Alliance akitoa tathimini fupi ya mashindano ya Future Rafiki Cup yaliyofanyika jijini Arusha.

Shangwe mashabiki wakichukuwa pix na kombe lao.

Msafara wa Alliance School Academy kuelekea katikati ya jiji na viunga vyake kuvionyesha vikombe vyake vya ubingwa U-14 na U-17.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.