ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 21, 2012

MAMIA WASHIRIKI KUMZIKA MCH. JAMES KWAKA OLIMO

Mamia ya wananchi toka sehemu mbalimbali leo wamejitokeza kwa wingi katika kijiji cha Kiabakari mkoani Mara kumzika Mchungaji Mstaafu kipenzi cha watu James Kwaka Olimo wa Kanisa la Menonite mkoa wa Mara aliyefariki dunia mnamo jumamosi ya wiki iliyopita tarehe 13july2012 katika Hospitali ya Rufaa Bugando ambako alikuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa leo tarehe 21july2012.

Watoto na ndugu wa marehemu katika picha ya pamoja nje ya kanisa la Menonite jimbo la Musoma mjini ambapo ibada ya kuuaga mwili wa marehemu mchungaji mstaafu Olimo ilifanyika.


Wachungaji wakiwakilisha kanda mbalimbali nchini wamehudhuria ibada hii takatifu.


Huzuni na majonzi vilitawala ndani ya kanisa la Menonite Musoma Mjini pale watoto wa marehemu walipokaribia mwili wa mpendwa baba yao kwaajili ya kutoa heshima za mwisho.


Waumini ndani ya Kanisa la Menonite Musoma mkoani Mara wakishiriki ibada hiyo.


Wachungaji na Maaskofu zaidi ya 50 toka makanisa mbalimbali nchini wameshiriki ibada hiyo hii leo.


Wachungaji na Maaskofu wakiwa wameubebe mwili wa mpendwa wao kutoka kanisani tayari kwa safari kuelekea Nyumbani kwa ukoo wa marehemu eneo la Kiabakari kwa ajili ya maziko.


Mwili wa marehemu Mchungaji Mstaafu Olimo, uliwasili kijiji cha Kiabakari majira ya saa nane hivi na kukutana na Ummati mkubwa wa waombolezaji.


Marafiki na wazee wa kaya mbalimbali eneo la Kiabakari.


Mwili wa marehemu Mchungaji Mstaafu James Kwaka Olimo ukishushwa kaburini kwa heshima na taratibu za kanisa wahusika wakiwa ni wachungaji waliohudhuria toka makanisa mbalimbali.


Marafiki wakishuhudia yanayojiri kwa safari ya mpendwa wao.


Kamera yako haikupata jukwaa kuonyesha picha kamili ya Umma ulioshiriki maziko hayo lakini ilipenya na kuona japo engo hii.


 Kamera yako  iliwasihi Mabinti hawa wa marehemu 'japo watabasamu' kwani baba yao waliyempenda katwaliwa na yule aliyemleta mara baada ya kumaliza kazi yake duniani, nao wakatabasamu kujifariji.


Picha ya pamoja na mzee mkongwe wa ukoo.


Wakufunzi wa Chuo Cha Ualimu  Bunda ambao ni mashabiki namba moja wa www.gsengo.blogspot.com nao walihudhuria mazishi hayo, kutoka kulia Alex Mwingira, Emmanuel Mandango, Jublet Shuma, Hilary Majimbe na Tumaini Mnale.


Kutoka kushoto ni Edgar Mapande, G. Sengo na Mr Ben.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.