ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 1, 2012

DAWA YA NGUVU ZA KIUME PART TWO

Kwanza poleni na majukumu ya wiki nzima ya kupambana na maisha na wale waliopo ofisini hata leo jumamosi pia niwape pole kwa kupambana na maisha. Nimekuwa nikifuatilia kila nikipata fulsa kusoma hii mada inayohusu NGUVU ZA KIUME.
Naambatanisha picha ya muonekano wa supu ya Aspergers ili ukienda kwenye super market uweze kuitambua. Hii inapatikana kwenye super market na maduka madogo.
 
Labda niingie kidogo kuongeza ninayoyajua,nguvu za kiume ni asili ya mtu kuwa na nguvu hizo na sio madawa kama tunavyodhani. Mtu unaweza kuwa na nguvu za kiume tokea ujana wako mpaka unapofikia uzee wako.Kuna baadhi ya vijana hukosa nguvu za kiume kwa sababu kadhaa na kadhaa. Wengi wa watu hukosa nguvu za kiume kwa kuwa na msongo mkubwa wa mawazo na wengine hukosa nguvu za kiume kwa kufanya kazi nzito.

Watu wenye msongo wa mawazo hukosa nguvu za kiume kwa kuwa kila dakika iendayo kwa MUNGU wao huwa na stress zao ambazo haziepukiki.Na kuna watu huwa wanafanya kazi ngumu sana kutokana na ugumu wa maisha bila kujua kuwa kazi zile zinawasababishia kupoteza nguvu za kiume.Kwa upande wa vijana wengi wale wanaopendelea kuangalia picha au video za (x) hupoteza nguvu zao bila kujielewa.

Kwa wale wanaofanya kazi nzito kama kubeba mizigo mizito au kufanya kazi kwa muda mrefu nao hupoteza nguvu zao bila ya wao kujielewa, hata kwa wafanyakazi wa maofisini kadhalika kwa kukaa kwa muda mrefu kwenye viti vyao hupoteza nguvu za kiume bila wao kujielewa.

VICHOCHEO VYA NGUVU ZA KIUME.
Kuna baadhi ya waungwana wamejaribu kutuwekea baadhi ya vyakula/vinywaji kwa kusema vinaongeza nguvu za kiume...kwa upande wangu siwezi kubisha kwamba haviongezi nguvu za kiume ila mtazamo wangu ni kwamba hivyo ni vichocheo vya hisia za mapenzi na sio 100% kwamba vinaongeza nguvu za kiume.Nguvu za kiume ni asili ya mtu na jinsi unavyoujali mwili wako.nikisema kuujali mwili wako nina maana kwamba unapokula vizuri na kuupa muda wa kutosha mwili wako basi always utajikuta hukosi nguvu za kutosha za starehe ya tendo la ndoa.

Jitahidi sana kuupa mwili mapumziko ya kutosha,fanya mazoezi mara kwa mara kwani mazoezi ni moja ya kigezo cha kufanya mapenzi kwa kutumia nguvu ukiwa huna nguvu za kutosha hutaweza kufanya mapenzi kwa ubora na kiwango cha kuridhisha. Nikisema nguvu sina maana unapofanya mapenzi lazima uwe na mabavu ya kumtimbatimba mwenza wako lahasha... nina maana ukiwa na pumzi ya kutosha utakuwa na uwezo wa kuyafurahia mapenzi kwa kuwa utatumia muda wa kutosha kumfikisha mwenza wako na wewe ukamaliza kwa muda muafaka bila kuvunja rekodi ya dunia.

ASPERGERS SOEP
Kuna kichocheo hiki ambacho sio siri ni kizuri sana endapo utakuwa unakunywa kila siku au mara kwa mara. Ni supu ambayo hata mimi napendelea kuitumia kila weekend hata leo asubuhi nimeitumia,jina la Supu hiyo ni ASPERGERS kwa yoyote mwenye kupenda kuwa na kichocheo cha mwili wake kuufanya uwe na hisia za mapenzi basi ajaribu kunywa supu hiyo.Ila ni vyema kwa wale wana ndoa kama mimi kwani awe na uhakika kwamba usiku au baadae anaingia shambani kulima vinginevyo itakupa tabu sana kwani ina kichocheo kikubwa sana mwilini.

TAHADHALI
Kwa wale wanaopenda kutumia madawa ya kuongeza nguvu za kiume,Binafsi nawashauri sio vyema kabisa kwani madhara yake ni makubwa sana kulinganisha na faida unayoipata kwa muda mfupi. Unaharibu moyo bila kujua na ukiwa sugu wa kutumia madawa hayo kumbuka siku za usoni kupoteza kabisa nguvu hizo za kume na kuukaribisha upofu.

USHAURI WA BURE
Mapenzi ni starehe hivyo kina baba wenzangu tuyafanye kwa sterehe na sio kama unamkomoa huyo mwenza,tujaribu kufanya mapenzi kwa hamu na sio shibe.Maana kuna baadhi ya watu wanatafuta madawa ya kuongeza nguvu ili wakakomoe..mapenzi huwezi katu kumkomoa mwenza ila unapoteza nguvu nyingi kwa kuwa unatumia nguvu nyingi.

Huu ni ushauri wangu na maoni yangu kwenu ila kama kutakuwa na mapungufu niwatake radhi. Ahsanteni sana na nawatakia jumamosi njema.

By Maganga One

Tupe maoni yako

3 comments:

 1. hii dsoup inapatikana wapi?

  ReplyDelete
 2. Kaka yangu, mm cna msichana kabisa na ninahtaji kuwa na msichana ila kila ninae mfata anasema anamtu, so naomba ushauri wenu ndugu zangu!

  ReplyDelete
  Replies
  1. Shukuru ata hao wanao kwambia wanamtu, wengine watakuchuna na badae utakuja kugundua kuwa ana mtu. Unayo bahat ya kuambiwa ukweli. Usikate tamaa ipo siku utapata wako omba Mungu atakusaidia.

   Delete

Note: Only a member of this blog may post a comment.