ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 1, 2012

MISS UNIVERSE 2011 ‘NELLY KAMWELU’ KUCHANGIA MFUKO WA SARATANI YA MATITI

 
MISS UNIVERSE 2011 ‘NELLY KAMWELU’ KUCHANGIA MFUKO WA SARATANI YA MATITI

Mrembo anayeshikilia taji la Miss Universe Tanzania 2011/2012 Nelly Kamwelu kwa kushirikiana na Mfuko wa Saratani ya Matiti Tanzania (Breast Cancer Foundation) wameandaa hafla kwa ajili ya harambee ya kuchangia mfuko wa saratani ya matiti itakayofanyika tarehe 1/6/2012 siku ya Ijumaa katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni hadi saa nne usiku.

Vilevile katika hafla hiyo kutakuwa na mnada wa kito cha Tanzanite ambayo imetolewa maalum na kampuni ya Richland Resources kwa ajili ya kuchangia mfuko huu. Pia picha ya Mrembo wa Miss Universe Tanzania itanadiwa katika mnada huo.

Mrembo Nelly Kamwelu toka achukue taji la Miss Universe Tanzania 2011, amekuwa akifanya kazi bega kwa bega na mfuko wa saratani ya matiti ikiwamo kusaidia kutoa elimu katika shule mbalimbali ili kupunguza au kutokomeza uwezekano wa kuenea kwa saratani ya matiti. Mfuko huu umepanga kuendeleza elimu hii kwa shule za mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Iringa, Mtwara na Lindi.

Kwa kusindikiza hafla hii kutakuwa na maonyesho ya mavazi yaliyotolewa na wabunifu wa hapahapa nchini ambao ni Escado Bird, Kemi Kalikawe na Subira Wahure vilevile kutakuwa na burudani ya muziki kutoka msanii Enika na mchekeshaji Evans Bukuku. Pia mrembo mwenyewe Nelly Kamwelu atatoa burudani ya dansi aina ya Belly Dance.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na waandaji wa Miss Universe Tanzania tell: 0714 441165 Mwanakombo Salim (Mratibu wa Kitaifa)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.