ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 23, 2012

MASHALI V/S SAMSON ULINGONI-Friends Corner Hotel jumapili

 Mabondia Thomas Mashali na Maisha Samson wamemaliza zoezi zima la upimaji na tayari kwa ajili ya mpambano wao utakao fanyika katika ukumbi wa Friends corner hotel-manzese siku ya jumapili 24/6/2012.

Mpambano huo wa ubingwa wa taifa wa TPBO uzito wa midle na unaosimamiwa na TPBO chini ya rais wake Yasin Abdallah na katibu mkuu Ibrahim Kamwe umemalizika vizuri na mabondia wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa fight.

Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Ibrahim kamwe na kueleza kuwa mabondia hao wote wawili kwa pamoja wamepata @kilo 71 na watacheza raundi kumi.
Pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kama ifuatavyo;
Juma Fundi (52kg) v/s shaban madilu (49.5kg) - watacheza raundi nane
Mohamed Shaban'ndonga' (61kg) vs Musa hassan (61kgs) - watacheza raundi sita
Jonas godfrey (61.5kgs) vs Venance mponji(59kg) - watacheza raundi sita
Abdalah mohamed'prince naseem'(64kgs) vs Yohana Mathayo(65.5kgs)- raundi sita
Nasoro Hatibu 55kg vs Abdul Athuman 55kgs -watacheza raundi nne
Martin Richard 50kgs vs Hassan Kadenge 49kgs -watacheza raundi nne

Ngumi zitaanza kama kawaida kuanzia saa kumi jioni, na tunarudia tena kusema katika ngumi hakuna kupendelea na TPBO itasimamia kwa haki zote bila kuangalia mtu. tutakachoangalia ni mchezo kuchezwa kwa kanuni za ngumi na utoaji points kulingana na bondia anavyoscore kwa ngumi halali sio kulingana na makelele ya washabiki.


Wako
IBRAHIM ABBAS KAMWE-BigRight
Katibu Mkuu TPBO

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.