ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 23, 2012

DIWANI MABULA AKABIDHI BAJAJI YA KUBEBEA WAGONJWA KWA ZAHANATI YA SHADI

 Pichani diwani wa kata ya Mkolani Stanslaus Mabula akimkabidhi ufunguo wa bajaji ya  kubebea wagonjwa kwa mwenyekiti wa mtaa wa Shadi bw. Anthony Mabasi. Ni takribani miaka 22 wananchi wa mitaa ya Shadi, Luchelele kati, Luchelele Ziwani na Sweya kata ya Mkolani wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wamekuwa wakitaabika kupata usafiri kwa nyakati zote (mchana na usiku) kiasi cha kutembea zaidi ya km 14 kupata zingine.

Video diwani Mabula.

 Akipokea msaada huo mwenyekiti wa mtaa wa Shadi, Anthony Mabasi amempongeza diwani huyo kwa kujibidiisha hadi kufanikiwa kulitatua tatizo hilo lililokuwa likikikabili kijiji chake na kuahidi kushirikiana na watumishi wa zahanati hiyo kuitunza Ambullance hiyo ili iweze kutoa huduma kwa muda mrefu.

 Diwani wa kata ya Mkolani Stanslaus Mabula akijaribu Ambulance hiyo ya magurudumu matatu huku akiwa amembeba mwanakijiji wa Shadi aliyehudhuria makabidhiano hayo.

 Changamoto kubwa kwa Zahanati hiyo ilikuwa ni pale ilipokuwa ikipata wagonjwa wakiwemo wanawake wajawazito kufikishwa katika hospitali hiyo hasa nyakati za usiku huku wengine wakihitaji kupelekwa kwenye hospitali ya wilaya iliyoko Butimba umbali wa km 14 kupata tiba zaidi ambazo haziwezi kutatuliwa kwenye zahanati hiyo wengi walikuwa wakipoteza uhai kwa kukosa usafiri.

 Pamoja na kukabidhi Ambulance hiyo ya magurudumu matatu pia diwani huyo ametoa msaada wa mabenchi mawili madhubuti kwaajili ya watu wanao hudhuria kituo hicho cha afya.

 Picha ya pamoja.

Kutokana na msaada huo wagonjwa wote wakiwemo wajawazito watarahisishiwa kupata huduma ya usafiri bure iwapo wataamriwa kupelekwa hospitali ya wilaya kupata tiba zaidi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.