ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 17, 2012

WACHEZAJI SIMBA WAMLILIA PATRICK MAFISANGO

Mkurugenzi wa mtandao wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku kulia akimsikiliza Katibu Mkuu wa timu ya Simba Bw. Evodius Mtawala wakati alipokuwa akielezea mipango ya kuuhifadhi na kuusafirisha mwili wa mchezaji wao marehemu Patrck Mafisango Mutesa aliyeafiki alfajiri ya usiku wa kuamkia leo maeneo ya Chang'ombe Veta jijini Dar es salaam, wakati akirejea nyumbani kwake na kusababisha watu wengine aliokuwa nao kupata majeraha.

Bw. Mtawala amesema hayo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na kueleza kwamba kwa sasa wanawasiliana na Ubalozi wa Rwanda na mashirika ya ndege ili kukamilisha utaratibu wa vibali mbalimbali tayari kwa kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda nchini Rwanda kwa mazishi na taarifa kamili ya lini utasafirishwa itatolewa kesho mara baada ya kukamilika kwa taratibu zote, katika picha kushoto ni Bw. Mwakitalima mmoja wa mashabiki wa Simba aliyefika muhimbili kushuhudia kilichotokea.
Wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga kushoto na Uhuru Selemani wa Simba wakisikitika wasijue la kufanya baada ya kushuhudia mwili wa mchezaji mwenzao marehemu Patrick Mafisango katika chumba cha kuhifadhia maiti muhimbili leo.

Haruna Moshi akitoka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti huku akilia kwa uchungu baada ya kuhakikisha kweli mwenzao Patrick Mafisango amefariki.

Mchezaji wa zamani wa Simba Boniface Pawasa akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na Mchezaji haruna Niyonzima wa Yanga, Pawasa amesema jana walikuwa naye kwenye muziki katika klabu ya Maisha Oysterbay wakati bendi ya Akudo Impact ikifanya onyesho klabuni hapo na marehemu alimuaga kwamba anaenda nyumbani baadae akapigiwa simu kwa simu ya marehemu akiambiwa mwenye simu hii amefariki dunia kwa ajali.

Uhuru Selemani akisalimiana na wanamuziki wa bendi ya Akudo Impact ambao pia wameelezaea masikitiko yao kwani wamesema marehemu walikuwa naye usiku wa kuamkia leo katika klabu ya Maisha ambako walikuwa wakifanya onyesho lao.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili leo asubuhi.
Picha na Full Shangwe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.