Bodi ya mchezo wa ngumi nchini Uingereza ilikataa kuidhinisha pambano hilo, kwani mabondia wote wawili hawana leseni ya Uingereza inayowaruhusu kupambana.
Uamuzi kufuatia rufaa ya Dereck Chisora kutetea uamuzi wa kumpokonya leseni umecheleweshwa, na Frank Warren amekasirishwa sana na namna bodi ya Uingereza ya ngumi ilivyoshughulikia suala hilo. “Kwa wengi ni vigumu kuvumilia kuwaona Chisora na David Haye hatimaye wakinufaika kutokana na tukio la fedheha mjini Munich, lakini katika ngumi, tukio kama hilo ni chanzo cha pambano la kusisimua zaidi litakaloweza kufanyika katika nchi hii”.
Chisora alipokonywa leseni kufuatia matukio kadha kabla na baada ya pambano lake dhidi ya Klitschko. Kati ya matukio hayo, Chisora, mwenye umri wa miaka 28, alimpiga kofi Klitschko kutoka Ukraine, wakati mabondia hao wawili walipokuwa wakipimwa uzani, na kisha kumtemea maji ndugu yake, Wladimir, kabla ya pambano hilo.
Kwa upande wake, Haye aliisalimisha leseni yake mwezi Oktoba mwaka jana, miezi mitatu baada ya kushindwa na Wladimir mjini Hamburg, Ujerumani, katika pambano la kuwania mkanda wa WBA. Awali Warren alikuwa amesema hana nia ya kusimamia pambano kati ya Chisora na Haye. Lakini amesema amebadilisha nia, kwa kuona rufaa ya Chisora kutaka leseni sasa imesukumwa hadi mwezi Julai.
Warren anakiri kwamba alilofanya Chisora ni jambo la kipumbavu, na anastahili adhabu. Lakini anasema bondia huyo atakuwa nje ya ulingo miezi sita, na ana haki ya kujipatia pesa na riziki yake maishani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.