ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 5, 2012

HAPA NA PALE WILAYANI MULEBA MKOANI KAGERA

Mkoa wa Kagera ni moja kati ya mikoa hapa nchini inayoongoza kwa kutokuwa na maambukizi makubwa ya ugonjwa wa malaria pamoja na hilo serikali haijabweteka kuhakikisha kuwa inaangamiza kabisa mazalia ya mbu.. pichani bwana Jovita N.Ngambeki akitoa elimu kwa moja ya kaya (haionekani pichani) ili aanze zoezi la kupulizia dawa maarufu kwa jina 'Dawa ya ukoko'

Shughuli hizo za unyunyiziaji hufanywa kwa umakini mkubwa huku 'timulida' (team leader)  wakikagua mara baada ya unyunyiziaji kufanyika.

Jovita N.Ngambeki tayari kwa kuanza zoezi katika kijiji cha Ilogelo tarafa ya Kamachumu wilayani Muleba.

Serikali yetu iling'aka sana mara baada ya mchizani Sauper kutengeneza filamu ya DARWIN’S NIGHTMARE ambayo ndani yake ilionyesha watanzania wakitumia mabaki ya samaki maarufu kama mapanki kama mboga tegemeo huku minofu ya samaki iklisafirishwa tani kwa tani kuelekea nchi za wenyenazo kwaajili ya biashara. Pichani ni mokono ya mteja ikichambua mabaki ya samaki toka viwandani mara baada ya minofu kutolewa (mapanki)  yakiwa sokoni kwaajili ya mboga, katika Gulio la Kilamba linalofanyika kila jumapili kijijini Rwigembe.

Panki
Mimi msimamo wangu ninasisitiza kuwa mapanki ni kitoweo kinachoonekana kawaida familia kadhaa cha kila siku katika familia hizo kanda ya ziwa sio Mwanza tu hata Kagera wanakula 'Mapanki' bwana.

Mapanki yakiwa kwenye meza ya mchuuzi.
"Mimi mwenyewe nimeanza kula mapanki kuanzia mwisho mwa miaka ya tisi, Leo hii watu wanashangaa kitoweo cha Mapanki ila nimejikuta nakula mapanki kutokana na uhaba wa sangara" alisema mmoja kati ya wadau wa kijiji cha Rwigembe kilichopo kata ya Ngenge wilayani Muleba.

Ingawa hukaushwa mabaki mengine hutoa harufu ya kuharibika
Wadau nawasihi tuitizame upya filamu ile na ifanyiwe utafiti ili ukweli ujulikane kama mtunzi ana makosa au la. Nakumbuka juu ya sakata lile la filamu kuna udanganyifu ulifanywa toka kwa viongozi kwenda kwa prezidaa' kama walivyozoea kuwapotosha viongozi wengine wa kitaifa, kwamba mapanki yanaliwa na watu maskini tu...

Wananchi katika pilikapilika gulioni Kilamba linalofanyika kila jumapili.
Picha na mdau wa G. Sengo Blog bwana Samadu Abdul 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.