ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 28, 2012

YA WAZIRI MAIGE 'SHANGAA .... USISHANGAE'

Mjengo wenyewe.

Kipi hatari waliojenga mahekalu bila kukopa au walionunua kwa kukopa?
Usishangae asilimia kumi ya watu wanamiliki asilimia themanini ya uchumi wa dunia while the rest wanagombania makapi. Wakati kuna mtu ana struggle kwa mshahara wa laki mbili kuna mtu ananunua shati dola elfu moja na yuko Tanzania hii.

Kilo moja ya pamba ni shilingi mia tatu na hiyo kilo inaweza kutengeneza shati tano ambazo zikirudi Tz huuzwa kwa shilingi elfu hamsini mpaka laki nne kutegemeana na brands. Wakati wa Nyerere watu walitupa magunia ya hela lakini was it worth it?

Kama hizo hela wangeambiwa wajenge viwanda Tanzania hapa leo hii tungekuwa na akina Diallo wengi na ajira kibao kwa nchi na export kubwa. Kenya ya mabepari wakati huo wakiitwa manyang'au leo hii wanaweza kufinance budget yao kwa asilimia tisini na tano.

Sisi tuko wapi? Why Kenya? kwa sababu walijenga uwezo kwa wawekezaji wa ndani wakati sisi hata wale wasukuma waliohangaika au wachaga waliosota tuliwaweka rumande eti wahujumu na kutaifisha mali zao.

Leo hii nyumba za NHC wanakaa akina Pateli kwa kodi ya bure waswahili wako hoi huko mbagala and elsewhere.

Katika kupiga vita rushwa tuwe makini tusijikute tunasombwa na kimbunga cha mawazo hasi kwamba kila mtanzania anayepata basi kauza unga au kaiba au ni freemasons.
Hiyo ni hatari.

Copy & paste Kutoka kwa
fikra za mdau Rmg...2000

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.