ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 27, 2012

MCHEZO WA AND 1 NA MWANZA ALL STARS WASHINDIKANA KISA BOGI (MVUA)

Kukosekana kwa viwanja vya ndani vimeligharimu jiji la Mwanza kukosa burudani ya Kimataifa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa mchezo wa basketbal waliofurika katika dimba la CCM Kirumba hii leo mara baada ya mvua kubwa kunyesha hali iliyopelekea hali ya uwanja kuwa tete.
Mwanza All Stars

Maiko Maluwe ni Kaimu katibu mkuu shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania ambaye ameambatana na timu ya And 1 jijini Mwanza naye anaeleza sababu za katisho la mchezo huo... .

Huku mashabiki wa basketbal wa jiji hilo la miamba wakiwa na kiu ya kushuhudia maufundi ya wachezaji wa Mwanza All stars na wale wakali kutoka nchini marekani And 1, ilikuwa ni majira ya kumi mvua kubwa ilinyesha kwa muda mrefu hata kusababisha eneo la uwanja kuwa si salama kwa wachezaji.
Ground kabla ya bogi kushuka...
Wacheza mahiri wa timu ya mpira wa kikapu And 1 wakipasha misuli moto kabla ya mpambano.
Wachezaji wa And 1 wakijadiliana hatma ya mchezo wao mara baada ya hali ya hewa kuzingua dizaini.

"Yo men the rain is coming..."

Adam Mchovu na Reuben Ndege aka Ncha Kali (R) wakionyeshana maufundi.

Baba Joniii akipata flash na Blogu.

Wacheza wa And 1 wakishow love na mashabiki wao wa jiji la Mwanza.
Kiu haikuwa kwa mashabiki pekee bali pia kwa wachezaji wa nyumbani (Mwanza All Stars na hapa team captain Vicent Shinda anafunguka...

Yes we...

Mwanza All Stars katika mwonekano wa pili.

Mwanza All Stars na mashabiki wao wa nyumbani vizazi vijavyo katika game la kikapu, kiukweli Mwanza kama ni wachezaji wapo tatizo hakuna viwanja vya kutosha vilivyo rafiki kwa mchezo husika nikimaanisha visivyo tegemea mabadiliko ya hali ya hewa .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.