ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 30, 2012

TANZANIA INAONGOZA KUWA NAVIZUIZI VISIVYOFAA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI: MBUNGE MASHA

Tanzania inatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kuwa na vizuizi ving visivyofaa mipakani na katika sheria zake kuliko nchi nyingine zote Afrika Mashariki ambavyo vinasababisha watu wake kuzikosa fursa zilizopo ndani ya jumuiya hiyo, hayo yamebainishwa na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Dr.F.Lwanyantika Masha alipotembelea ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mwanza (MPC).

Pia mbunge huyo amesema kuwa watanzania wengi hawajapewa habari vya kutosha kuhusu fursa zilizopo ndani ya soko la nchi za Afrika Mashariki ili kuzichangamkia fursa zilizopo.

Dr.Masha ameshauri na kutia msisitizo kuwa badala ya kunung'unika Tanzania yapaswa kujiandaa na changamoto za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili wadau wake wasipwaye katika soko.


Makamu Mwenyekiti wa MPC Frola Magabe akisoma risala mbele ya Mh. Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Dr.F.Lwanyantika Masha alipotembelea ofisi ya Chama hicho chenye wanachama 130 jijini Mwanza anayefuata ni katibu wake E. Soko.

Ndani ya Mwezi April 2012, Dr.F.Lwanyantika Masha anategemea kuzindua vitabu vyake viwili MAJUKUMU YA MBUNGE na AZIMIO LA ARUSHA (alichokishika).

Picha ya pamoja.
Kuhusu MUUNGANO WA KISIASA Masha amesema kuwa moja kati ya makubaliano ya Shirikisho la Jumuiya ya Afrika mashariki ni kwamba hatimaye mara baada ya kuondoa Ushuru wa forodha, kuwa na Common Market, kuwa na Sarafu moja pamoja na mfumo wa fedha hatua itakayofuata ni kuwa na Shirikisho la kisiasa (POLITICAL FEDERATION) nayo mazungumzo tayari yamekwishaanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.