ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 9, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUSITISHWA MGOMO WA MADAKTARI


Kwa: Wahariri wote;
TV,
RADIO,
MAGAZETI,
BLOGU,
Leo, tarehe 8, Machi 2012, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, mbele ya Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza Ombi No. 24 la 2012 lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Mwombaji) dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari (Walalamikiwa), imetoa uamuzi ufuatao:

i) Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari pamoja na Wanachama wao, kusitisha Mgomo waliouanzisha rasmi tarehe 7 Machi 2012 nchi nzima na kurejea kazini mara moja kwa kuendelea na kazi zao kama kawaida, mara tu Amri hii itakapowafikia. Aidha, waombaji watatakiwa kutoa Kiapo cha kuthibitisha kwamba wamewasilisha Amri hiyo kwa Walalamikiwa na kuwasilisha Kiapo hicho Mahakama Kuu – Divisheni ya Kazi kesho tarehe 9,Mach 2012.

ii) Mara baada ya Amri hii kuwasilishwa kwa Walalamikiwa (Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari) watatakiwa kuwatangazia Wanachama wao kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa Mgomo huo Nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wa kuitisha Mgomo huo;

iii) Mahakama inaamuru pande zote mbili (Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania pamoja na Jumuiya ya Madaktari) kutumia fursa za Kisheria zilizopo katika kutatua Mgogoro wa Kikazi uliopo kati yao kwa haraka.
(mwisho)
Imetolewa na:

Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM.
Alhamisi Machi 8, 2012

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.