ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 1, 2012

WAFANYABIASHARA WATOA MATAIRI 50 KWAAJILI YA MAKARANDINGA JESHI LA POLISI MWANZA

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow akikabidhiwa rasmi mchango wa matairi 50 yaliyotolewa asubuhi ya leo na mfanyabiashara maarufu Zuri Nanji kwaajili ya makarandinga ya jeshi hilo.

Mfanyabiashara Zuri Nanji amesema kuwa msaada huo ni kielelezo tosha cha utendaji bora wa jeshi la polisi Mwanza na amesihi jeshi hilo kuendeleza sera yake ya ulinzi shirikishi.

Kamanda Barlow akikagua umadhubuti wa matairi hayo yenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 20.

Sehemu ya maafisa wa jeshi la polisi walioshiriki makabidhiano hayo yaliyofanyika mbele ya ofisi za jeshi la polisi Mwanza.

Mfanyabiashara maarufu Josephat Musukuma (anayezungumza) alitoa shilingi milioni moja kwaajili ya mfuko wa magari ya doria ambayo yamekuwa yakikumbwa na kadhia ya kukwama kufika sehemu za matukio kutokana na uhaba wa mafuta sambamba naye Mfanyabiashara Riziki Mbise wa Kampuni ya Mambo ya Chinga Investiment (katikati) akikabidhi mchango wake wa milioni moja taslimu kwa katibu wake wa mfuko wa wafanyabiashara kwenda kwa jeshi la polisi.

Kamanda wa kikosi cha Doria na Ulinzi shirikishi Philip Karage akitoa shukurani kwa mchango huo.

'KITU KASHATA MMmma' ni karandinga lililofungwa tairi zote mpya.

Naye mfanyabiasha Rashid alitoa lita 400 za mafuta kwaajili ya vyombo vya doria, msaada huo utalinusuru jeshi la polisi na aibu ya makarandinga yake na pancha za mara kwa mara wakati wa safari zake pamoja na kukwama kutokana na uhaba wa mafuta.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.