ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 4, 2012

YOUSSOU N'DOUR ATANGAZA KUWANIA UPREZIDA'H

Mwanamuziki mashuhuri nchini Senegal na mwanaharakati wa kisiasa,Youssou N'dour, ametangaza kuwa atawania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi Februari nchini humo. Mwanamuziki huyo amesema kuwa anaitikia wito wa kumtaka agombee kiti hicho dhidi ya rais wa sasa Abdoulaye Wade, ambaye anapania kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu.

Youssou N'dour amehusika na maswala ya kibinadamu kwa siku nyingi na pia ni balozi wa shirika la umoja wa matataifa kuhusu maswala ya watoto (UNICEF).

Mwandishi wa BBC mjini Dakar, Thomas Fessy, anasema hatua ya bwana Youssou N'dour kutangaza kuwa atawania kiti cha urais, haijawashangaza wengi. Hii ni kufuatia tangazo alilotoa mwisho wa mwaka uliopita kuwa atajitosa katika ulingo wa kisiasa.

Katika hotuba iliyopeperushwa kupitia kituo chake cha redio na televisheni, mwanamuziki huyo amesema atapunguza matuzi ya serikali na kuahidi kuzalisha chakula na umeme kwa wote iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Senegal.

''kuwa rais ni kazi sio taaluma''Youssou N'dour anakubali kuwa yeye sio msomi lakini anaelezea wadhifa wa rais kama ''kazi na sio taaluma''.

Youssou N'dour alikuwa rafiki wa karibu wa rais Abdoulaye Wade, lakini baada ya Wade kutangaza nia ya kuwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu, aligeuka na kuwa mpinzani wake mkuu. Lakini haitakuwa kazi rahisi kwa Bw. Youssou Ndour kuwabadili maelfu ya wafuasi wake wa muziki kumpigia kura.

Aidha, Youssou N'dour amewahi kuwashutumu viongozi wa nchi za Afrika kuhusu jinsi walivyoshughulikia janga la njaa nchini Somalia.


CHANZO bbc swahili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.