ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 13, 2012

GOR MAHIA YASAJILI 6WAPYA IVO MAPUNDA NDANI

Katika kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini Kenya, timu ya soka ya Gor Mahia leo imetambulisha wachezaji wake sita wapya iliyosajili kwaajili ya msimu mpya unaotazamiwa kuanza wiki chache zijazo akiwemo golikipa wa zamani wa Tanzania (Taifa Stars) Ivo Mapunda.Mshambuliaji George Midenyo (pichani) amenyakuliwa na Gor Mahia toka timu ya Tusker ya nchini humo, Ivo Mapunda na mwenzake Rama Salim wamesajiliwa kutoka Congo United, wengine ni Yusuf Juma kutoka Thika United, Ali Hassan na Hugo Nzoka toka Sony Sugar.

Gor Mahia safari hii imejizatiti kufukuzia hatimaye kuyanyakuwa mataji yote matatu nchini humo likiwemo kombe la ligi kuu ya KPL, KFK Cup na KPL Top 8 trophy.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.