ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 17, 2011

MAONYESHO YA AJIRA SEKTA YA AFYA KWA HALMASHAURI YA MKOA WA MWANZA

Maonyesho ya ajira sekta ya Afya kwa halmashauri ya mkoa wa Mwanza na nyinginezo yamefanyika wilayani sengerema mkoani Mwanza. Lengo ni kuwatambulisha wanafunzi wa sekta ya Afya kuhusu nafasi za kazi zilizopo katika Halmashauri ya mkoa wa Mwanza ambapo maafisa ajira toka Halmashauri zote walikusanyika wilayani hapa na kuziainisha nafasi zilizopo kwenye wilaya zao. mfano Wataalam wa maabara, wauguzi, katibu afya na nyinginezo.

Katibu Tawala Msaidizi - Utawala na Utumishi Crecensia Joseph akitoa hotuba ya ufunguzi.

Field Zonal Cordinator wa Benjamin Mkapa HIV AIDS Foundation Remmy Moshi akitoa maelezo kuhusiana na kusudio la Taasisi hiyo kuziainisha nafasi za ajira sekta ya Afya.

Katibu wa Afya Wilaya ya Misungwi
Wadau hao wa Sekta ya Afya walipata fursa ya kuandika majina yao kwa wilaya walizotaka kufanya kazi pamoja na anuwani, mawasiliano ili pindi mchakato utakapo kamilika waitwe kwaajili ya kufanya kazi.

Katibu wa Afya Wilaya ya Geita Maganga H. Mwita akitoa maelezo na vivutio vilivyopo toka wilaya yake.

Ongezeko la ajira katika sekta ya afya inaonekana kukuwa toka 7,634 katika mwaka wa fedha 20007/2008 hadi 9391 kwa mwaka 2010/2011.

Hii inatokana na mkakati huu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamiii wa kupeleka moja kwa moja wahitimu kutoka vyuoni kwenda vituo vya kazi.

Toka wilayani Sengerema kuna nafasi nyingi za ajira kama vile Asst.Env.Health Officer ii(4), Asst. Medical Officer ii (3), Nursing Officer ii (1), Asst. Technologist ii (18), Clinical Asst (6), Health Secretary ii (1), Technologist ii (4), Medical Attendant (8), Nurse ii (16), Nutrition Officer ii (1), Pharmacist ii (1), Phsiotherapist ii (114), Technologist ii (1).

Katibu wa Ukerewe Ester Marick akitoa maelezo ya nafasi za ajira na vivutio vilivyopo katika halmashauri hiyo.

Vile vile Wizara inatekeleza mpango wa kukuza taaluma kwa njia ya masafa (Distance Learning); Tabibu Msaidizi kuwa Tabibu na Muuguzi kuwa Afisa Muuguzi Msaidizi.

Yote haya yanafanyika kama sehemu ya maboresho katika sekta ya Afya na ajira.

Thursday, December 15, 2011

MBUNGE WA ILEMELA AKUTANA NA MADEREVA WA PIKIPIKI MWANZA

Mbunge wa Ilemela Highness Samson Kiwia.
Uongozi wa Bodi ya Waendesha pikipiki jijini Mwanza leo umekutana na wadau wake, jeshi la polisi na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mbunge wa Ilemela kwaajili ya kuzungumzia mstakabari mziwa wa hali ya waendesha pikipiki.

Changamoto mbalimbali zimejadiliwa suala kuu likiwa ni Uvunjifu wa Sheria, ambao umepelekea kusababisha madhara makubwa kwa jamii hususani vifo kwa madereva wenyewe au kwa abiria ambao wamekuwa wakiwabeba.

Tatizo sugu la rushwa nalo lilijadiliwa kwenye mkutano huo uliofurika madereva wa pikipiki.

Elimu ya usalama barabarani nayo ilitolewa kuelimisha madereva wa pikipiki ili kuendesha kwa usalama kwa kuzingatia kanuni.

Vuta picha juu ya umati huu, wote hawa ni madreva wa pikipiki, kwa ukata wa ajira unaoliyumbisha taifa letu, Jeh bila wao kuwekeza kwenye biashara hiyo wote hawa wangekuwa wapi?

WANA MWANZA DAR MPOooooooo?

Wadau wa mwanza timu ya mpira wa kikapu mkoa wa mwanza (rocky city team) ipo katika mashindano ya Taifa cup jijini dar. Mpaka sasa timu hiyo imeshacheza mechi 2, mechi ya kwanza ilikuwa dhidi ya Zanzibar ambapo Zanzibar walishinda vikapu 56 vs Mwanza 55,game ya pili Mwanza iliigagadua Tanga kwa jumla ya vikapu 71 vs 40, Leo Mwanza imeshuka uwanjani kupepetana na timu ya mkoa wa Rukwa iwapo itashinda basi itakuwa ni tiketi kuingia hatua ya robo fainali.

Robo fainali itaendelea kesho sambamba na nusu fainali na fainali itakuwa jumamosi.
Uongozi wa basketball wa mkoa wa Mwanza unatoa wito kwa wana mwanza wote popote walipo hasa waliopo jijini Dar wajitokeze kwa wingi kuipa support timu yao ya mkoa iwe kwa hali na mali ukizingatia inakabiliwa na ukata kwani wadhamini TBL kupitia Castle lite wametoa shilingi laki 9 tu kwa kila timu hivyo gharama zingine ni juu ya mkoa wenyewe.

Hima hima mwenye maji ya kunywa ayaa, chakula ayaa, nauli ayaa na kulala pia. Timu inaishi Topland hotel Magomeni Mapipa na viwanja vya mashindano ni Don Bosco Upanga na Leaders Club.


Ni chini ya coach Robert Mwita, Timu ya mkoa wa Mwanza inaundwa na wachezaji Bundala Charles, Enock Charles, Ahmed Said, Vincent Shinda, Francis Shilinde, Wilson Sajigwa Masanja, Adam Jegame, Juma Kissoky, Mahamed Ally Dibo, Amri Mohamed, Amon Diba Semberya, Chacha Mukolo Tubert na Kizito Sosho Bahati.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA WATANGAZA HABARI NJEMA KWA WATANZANIA

Wakati wa kuadhimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara Ubalozi wetu nchini Uingereza ukishirikiana na Chuo Kikuu cha mji Coventry wanapenda kuwatangazia wadau wote wa elimu kuwepo kwa Scholarship sita maalum za masomo kwa watanzania ambazo zimetolewa kutoka katika Chuo kikuu cha Coventry katika nyanja zifuatazo:

1. MSc Oil & Gas Management
Coventry Campus
Kuanzia Septemba 2012

2. MBA Oil & Gas Management
London Campus
Kuanzia April, July, Septemba 2012

3. MSc Finance & Investment
IAA Dar Campus
Kuanzia Septemba 2012

4. MBA Logistics
IAA Dar Campus
Kuanzia Septemba

5. MSc Finance & Investment
IAA Arusha Campus
Kuanzia Septemba 2012

6. MBA Logistics
IAA Arusha Campus
Kuanzia Septemba 2012

Jinsi ya kujiandikisha, tembelea tovuti ifuatayo:

http://www.coventry.ac.uk/tanzania2012scholarship

ZAIDI ya hayo Ubalozi wetu ukiwakilishwa na Balozi Mh Peter kallaghe, Chabaka Kilumanga na Allen Kuzilwa, ulipata fursa pekee ya kukutana na kumpongeza afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndg. Semu Mwakyanjala ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya Pili( Masters Degree in Communication, culture & Media) katika chuo kikuu cha Coventry alieshinda tuzo ya kuandika insha kuelezea jinsi gani nchi ya Ujerumani itakavyokua mwaka 2051.

Aidha Mh. Balozi Kallaghe alimpongeza sana Afisa Semu kwa juhudi zake kwa kufanikiwa kushinda tuzo hii na kuiletea heshima Tanzania Ughaibuni na kuwahamisisha watanzania wote kusoma na kufanya kazi kwa bidii zaidi. Wakati akiongea na waandishi wa Habari afisa Semu alianza kwa kutoa shukrani kwa familia yake, wafanyakazi wenzake kutoka TCRA na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kumwezesha kufikia hatua aliyopiga leo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na ubalozi wetu hapa London 00 44 20 7569 1470

Tafadhalini watanzania wote chukueni hii nafasi mapema iwezekanavyo kwa wale wote mnaopenda kujiendeleza kimasomo.

Tuesday, December 13, 2011

WAZAZI KUKOSA NAFASI YA KULEA WATOTO ---> CHANZO CHA WATOTO KUHARIBIKA

Grace Massawe.
Warsha ya siku tatu ya kukusanya maoni ya wadau kuhusu hali ya maisha ya mtoto anayeishi mazingira ya mijini inayofanyika jijini Mwanza imebaini kuwa, Athari nyingi zinatajwa kuwa zitaendelea kuwakumba watoto wengi nchini kutokana na wazazi wengi kukosa nafasi ya kuwalea watoto katika makuzi bora sambamba na kuwaacha bila malezi.

Akina mama wengi huondoka kwenda kwenye biashara ndogondogo na kurudi nyumbani usiku, mchana kutwa hayupo nyumbani mtoto anaamka anapaswa kwenda shule hajapata kifungua kinywa, mchana anarudi nyumbani hakuna chakula, anaamua kutinga mtaani kusaka cha kutia tumboni. Huko anakutana na changamoto nyingi zenye madhara.

Wanawarsha.
Taarifa zinakusanywa hapa ili baadae zijumuishwe kwenye mpango mkakati wa UNISEF kusaidia watoto kutoka kwenye lindi la manyanyaso ili waishi maisha stahiki.

Afisa Mtendaji kata ya Mbugani Baruan Awadhi.
Mazingira ya nyumbani yanaweza kuwa si rafiki kwa mtoto yaani hayatoi fursa kwa mtoto kujisikia kuwa yuko huru kupata huduma nzuri toka kwa wazazi ikiwemo kusikilizwa.

Sehemu ya wakusanyaji maoni kwenye warsha hiyo.

Jeshi la Polisi nalo limehusishwa.
Serikali imeweka mpango kwa kila kata kuwa na askari kwaajili ya kupata taarifa juu ya mipango yote ya uhalifu.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mwanza, Stella Mbura
Wadau wajikite kwenye stadi za malezi ya watoto ili kuwanusuru watoto dhidi ya tabia chafu zitakazo isababisha nchi kupoteza uelekeo wa maisha ya baadaye.

Lengo kuu la shirika hili la hiyari linalojihusisha na harakati za kulinda na kutetea haki za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na magumu ni kutetea hadhi na haki ya watoto nchini Tanzania.

NDUGU ZANGU TUCHORWE TUPAMBWE MAJUMBANI

Picha namba Moko'

Picha namba Bee yenye kwesicheni'
Hebu tunyetishe nani Kapatiwaaa!!

PARTY YA KUZALIWA MTANGAZAJI WA STAR TV

Huu ndiyo Mkate wa nakshi ya sukari wa Fatma Shemweta katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika ukumbi wa VIP The New Stone Club Mwanza.

Mtangazaji wa Star Tv Fatma Shemweta (R) na shosti wake The Platnum (L).

ZE MilipukozZZZz!!

ChiazZZZzzz!!!

Kitu cha Dance' pale kati.

Kutoshea idadi keki ilikatwa 'mapande makumi mawili na saba'.

Fatma akilishwa keki na Beste'.

To the shosti.

To the Mc Ray.

Tamu ya mkate wa sukari kwa Mamaa G.

Meneja wa The New Stone Club, Dj Ally Coco naye alionja utamu wa keki.

Keki kwa dada.

The Big Top Ten akilishwa keki.

Platinum na shukurani kwa mtoto.

Mtoto akipokea zawadi spesheli.

Mc wa shughuli alikuwa na mikogo kinomanoma, na hili ndilo pozi la kukabidhi mzigo.

The Crew na Sahara Communication.

Safu ya mashosti...

Picha zaidi tembelea
www.jipanguse.blogspot.com

DUNIA KIZUNGUMKUTI WALIOUAWA SYRIA WAFIKIA 5,000

Zaidi ya watu 5,000 wanaaminika kuuawa katika maandamano ya nchini Syria, afisa wa ngazi za juu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa amesema.Pillay amewaambia wajumbe wa Baraza la Usalama kuwa watu 14,000 wanaaminika kukamatwa na wengine 12,400 wamekimbia hadi katika nchi jirani.

Takriban watu 20 waliuawa katika makabiliano ya siku ya Jumatatu. Licha ya fujo, uchaguzi ulifanyika, lakini idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura inasemekana kuwa ndogo.

Serikali inasema kuwa uchaguzi umekuwa huru zaidi kuliko miaka iliopita, lakini upinzani ulitoa wito wa kususia uchaguzi na kuanzisha mgomo.

Shirika la habari la serikali nchini Syria linasema watu wengi wamejitokeza katika vituo vya kupiga kura, Lakini katika ngome za upinzani wanaharakati wanasema hakuna dalili kama uchaguzi unafanyika, na hata pengine hakuna hata mmoja anayepiga kura, mwandishi wa BBC Jonathan Head aliye nchi jirani ya Uturuki anasema.

Navi Pillay anaelezea hali nchini Syria kama "isiyoweza kuvumiliwa" na kusema kuwa mateso dhidi ya binaadamu huenda yalifanyika.

Bi Pillay anasema makadirio yake ya mauaji ya watu zaidi ya 5,000 hayajumuishi maafisa wa usalama. Serikali ya Syria inasema kuwa zaidi ya maafisa 1,000 wa polisi na jeshi wameuawa.

Chanzo bbc swahili

Monday, December 12, 2011

HAPPY BAZDEI YA KUZALIWA FATMA SHEMWETA

Waungwana leo ni BorzDEi ya mtangazaji wa Star Tv FATMA SHAMWETA kama mna namba yake mpigieni mumpongezezZ!! Au kama vipi tupa makomenti... Kwani siku yake muhimu maishani.... Blogu hii na wadau wake wa ukweli inakutakia kila la kheri katika harakati za maisha yako Inshahlah Mwenyezi Mungu akujazie kheri kwa kila jema ulipangalo.

STONE CLUB NA WIKIENDI WE ACHA TU......!

Kama ni ngoma basi katika 1'N'2 Dj Ally B' anawakilisha.

Burudani ful-kiwango toka bOnGo lANd nazo hazikosi.

Mkali toka Tip Top Conection Tunda man akisanukisha.

Ming'aro na Ze crowd.

FrenDz toka Sahara Communication wakipata Flash ya pamoja.

Kaunta ya juu.

'Tukikwaituka' Mie na Rogers wa 'ROVING DJ' Star Tv.