ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 3, 2011

RASHIDI MATUMLA 'MTOA SUMU' AJIFUA KUMKABILI MANENO OSWARD 'MTAMBO WA GONGO DESEMBA 25

Bondia Rashidi Matumla (kulia) akioneshana ufundi wa kutupa masubwi na Mohamedi Matumla wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano na bondia Maneno Osward Desemba 25 katika ukumbi wa Henlken Kijichi Dar es salaam.

Ngumi ndonga masubwi mwanzo mwisho.

Rashidi Matumla akiruka Kamba katika Kambi yake ya Mazoezi iliyopo Keko Dar es salaam leo.

Rashidi Matumla 'Mtoa Sumu' akipiga panch Bang wakati wa mazoezi yake kabla ya kumkabili bondia maneno Osward Desemba 25.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Friday, December 2, 2011

MWANANGU CUTHBERT NA WENZAKE WALA NONDO CHEKECHEA

Cuthbert A.G.Sengo.

Sabrina Samadu Abdul Mtoto wa Mfanyakazi mwenzangu akipokea shahada yake.

Sabrina na Shukurani kwa mgeni rasmi.

Mtoto umleavyo ndivyo akuwavyo, pindi azitizamapo picha hizi katika makuzi yake ni changamoto kuisaka elimu ya juu zaidi.

Cuthbert na kaka yake Cedrick wakipata flash.

Flash ya Cuthbert na Daddy

Maigizo tyme..

Wahitimu wakipata mpunga kwenye mahafali ya shule ya Chekechea jijini Mwanza.

Mpunga ukiendelea..

Cedrick akimkabidhi zawadi mdogo wake kama changamoto ya kufanya vyema kwenye safari yake kuisaka elimu ambayo ndiyo kwaaaanza imeanza.

MIAKA 12 YA KUZALIWA KWA CLOUDS FM RADIO YA WATU KIBAO...................................!

Bwiga wa Mbwiga na Timu ya Sports X-Tra akipata kipande cha keki huku akishuhudiwa na na Ephraim Kibonde, Edo Kumwembe na Shaffi Dauda.

12 years kwenye Industry.

Kutoka kushoto Kibonde, Edo Kumwembe, Shaffi Dauda, Mbwiga, Alex luambano, Joff Lea na Abdul Mohamed.

Kipindi cha XXL nacho kilijitanua mida yake kutoka shoto ni B.12, Bobb Jurnior, Madee na Dj Fetty.

Adam Mchomvu aka 'Baba JONIii' (R) akijitanua na Maunda Zoro (kati) naye Mwalimu wa Waalimu Banza Stone.

THE CREW wakipata flash.

Leo Tena si ndiyo hawa Gea Habib(L), Dina Marious(C) na Husna Abdul(R).

"Amka kumekuchaaaa" PJ(L), Babra Hassan(C) na Bonge(R).

Shughuli ilianzia asubuhi katika kipindi cha Power breakfast na Hapa PB ilikuwa ikiisha na wakatukaribisha timu leo tena.

WAZIRI MKUU MH. MIZENGO PINDA KUENDESHA HARAMBEE YA HOSPITALI YA BUGANDO MWANZA LEO

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda, leo anatarajiwa kuzuru jijini Mwanza kwa ajili ya kuendesha harambee ya kuchangisha sh. Bilioni moja katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando inayoadhimisha miaka 40 tangu ilipoanzishwa rasmi mnamo mwaka 1971.

Akithibitisha kuhusu ujio wa kiongozi huyo wa kiserikali Mkurugenzi wa Hospitali ya bugando Dk Charles majinge amesema fedha hizo zitatumika kujenga maabara ya Saratani hospitalini hapo ambayo inatajwa kuleta mapinduzi ya utabibu nchini pindi itakapokamilika.

Kwamujibu wa Mkurugenzi huyo wa Hospitali ya Bugando harambee hiyo itafanyika leo kuanzia saa moja kamili jioni katika ukumbi wa Hotel Gold Crest iliyopo katikati ya jiji la Mwanza.

Akifafanua zaidi Dr. Majinge amesema kuwa uongozi wa Hospitali hiyo unamatumaini kwamba malengo ya makusanyo yaliyokadiriwa yatafikiwa sanjari na kuzidi malengo yaliyotajwa.

MANAMUZIKI 'MR. EBBO' KAFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO

Marehemu Abbel Olemotika 'Mr .Ebbo' enzi za uhai wake amefariki dunia alfajiri ya leo Jijini Arusha.
Ni kwa mujibu wa Radio one kumepambazuka leo asubuhi.
Habari zikimtaja mwanamuziki huyo maarufu ambaye vilevile alikuwa ni mtayarishaji wa muziki aka producer kupitia Recoding label ya MOTIKA RECORDS, Mr ebbo amefariki dunia.

Mr Ebbo aliyefahamika sana kwa nyimbo ya Mi Mmasai bwana, Ganja bana na Kamongo(kideoni) umemfanya nini pegere. Amefariki usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa kipindi kirefu tangu alipokuwa mkoani Tanga ambako ndiko alikuwa akiishi pamoja na familia yake. Taarifa zaidi tutaendelea kuziwasilisha kupitia Blogu hii.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Thursday, December 1, 2011

NAKUTUA KWENYE TUKIO BbPWAAAAAH!!

Kitu cha mbogamboga sokoni...

Mbogamboga zilizo oshwa na kukatwa katwa zikiwa sokoni/yaani nunua, tupia kwenye sufuria, pika.

KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU TZ MWENGE WA UHURU KUPANDISHWA MLIMA KILIMANJARO

Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Walioketi toka kulia ni IGP Said Mwema, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange, Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda.

Mama Maria Nyerere na Mama Salma Kikwete na wageni wengine mashuhuri jukwaa kuu.

Rais kikwete akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio hizo mwaka huu.

Kikosi cha wataopandisha Mwenge wa Uhuru Mlima Kilimanjaro.

Rais Jakaya Kikwete akikabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange ambaye atawakabidhi wapandishaji mlima Kilimanjaro.

Viongozi wa wataopandisha Mwenge wa Uhuru Mlima kilimanjaro.

Rais Jakaya akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh Fatuma Mwassa na maafisa wake baada ya mkoa huo kuibuka mshindi wa jumla wa mikoa iliyofanya vyema katika mbio za mwenge kwa wingi wa miradi na maandalizi.

Umma.

KWAHERI MWANA HABARI MKONGWE DAVID WAKATI

Mtangazaji wa siku nyingi nchini Tanzania na mwasisi wa Shirika la Utangazaji la Tanganyika Broardcasting Cooparation (TBC) enzi hizo na Mkurugenzi wa kwanza mzawa wa Radio Tanzania Dar es salaam (RTD) Mzee David Wakati amefariki dunia alfajiri ya wa kuamkia leo jijini Dar-es-salaam katika hospitali ya Regency iliyopo maeneo ya Upanga,imefahamika.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa kutoka kwa ndugu wa karibu wa Mzee Wakati, mtangazaji huyo mkongwe, amefariki kutokana na maradhi ya kiarusi ambayo amekuwa akisumbuliwa nayo tangu mwaka jana. Mungu aiweke roho ya marehemu David Wakati mahali pema peponi AMEN


Marehemu David Wakati(wa kwanza kushoto) akiwa na waandishi na wanahabari wengine Ikulu jijini Dar-es-salaam walipokwenda kumuaga Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipotangaza kustaafu mwaka 1985.

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI MKOANI MWANZA

Maandamano ya wadau wanaojishughulisha na mapambano ya kudhibiti UKIMWI katika jiji la Mwanza yakiingia katika uwanja wa Nyamagana asubuhi hii.

Siku hii inatukumbusha kama sehemu ya jamii kupanga mikakati endelevu ya kuzuia Maambukizi mapya, kuzuia Unyanyapaa na kukabiliana na vifo vitokanavyo na UKIMWI.

"Kiwango cha maambukizi katika jiji la Mwanza kimeshuka toka 12% mwaka 1999 hadi 5.7% mwaka 2007 hii ni kutokana na ushirikiano wa dhati kati ya Halmashauri ya jiji na wadau wake" Ilisema sehemu ya risala toka kwa wadau wanaojihusisha na masuala ua Ukimwi katika maadhimisho siku ya Ukimwi duniani desemba mosi 2011.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Said Amanzi (shati la kitenge) akiwa na diwani wa kata ya Nyamagana Biku Khotecha kwenye Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
"Tathmini mbalimbali zinaonyesha kuwa bado kuna mianya ya mtu kuambukizwa VVU katika jamii kupitia ngono zembe na mtu aliyeambukizwa na VVU.

Sababu nyingine ni pamoja na mila na Desturi za kurithi wajane, Ulevi wa kupindukia na Umaskini kwa hiyo ili kupiga vita maambukizi mapya ya VVU mambo haya hayana budi kupigwa vita kwa gharama yoyote ile" amesema Mh. Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Said Amanzi.


Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inayosema 'Tanzania bila maambukizi mapya, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na ukimwi inawezekana' imelenga kuwahimiza wananchi kupima kwa hiari ili kujua afya zao na kwa wale watakaokutwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi basi waweze kuzingatia ushauri wa KITAALAMU hii itachangia katika kupunguza vifo vitokanavyo na UKIMWI.

Hata hivyo pamoja na Halmashauri ya jiji la Mwanza kujitahidi kukusanya asasi mbalimbali katika viwanja hivyo huku ikitumia raslimali fedha zinazopatikana toka kwa wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi, maadhimisho hayo hapa jijini kwa mwaka huu hayakuwa na mahudhurio ya kuridhisha kama miaka mingine, kiasi cha kuonekana kama asasi hizo zilikusanyika kupeana ujumbe wao kwa wao bila wananchi ambao ndiyo walengwa.

Wednesday, November 30, 2011

TWANGA MACHO MBELE MILTON KEYNES IJUMAA HII

Chalz Baba, Maria na Baby Tall wakiwa kwenye ukumbi wa wa Golden Lounge ndani ya Mji wa Milton Keynes kufanya Promo ya show yao ya Pili katika ukumbi wa Golden Lounge Milton Keynes UK, Ijumaa hii ya tarehe 2 desemba 2011

GARY SPEED HAKUWA NA UGOMVI NA MKEWE WALA KUONEKANA KUWA NA HUZUNI KABLA YA KIFO CHAKE.

Nyota wa Football ambaye alikuwa meneja wa timu ya taifa ya soka ya Wales, Speed ​​Gary hakuonekana kuwa na huzuni na hakuwa na ugomvi baina yake na mke wake Louise kabla ya kifo chake ambapo inasemekana alijiuwa mwenyewe, wakala wake amesema. Enzi za uhai wake Gary Speed na mkewe Louise.
Hayden Evans aliongeza kuwa: "Hata mke wa marehemu bado anatatizwa na kifo cha mumewe. Wameishi maisha ya upendo katika ndoa yenye furaha huku akimchukulia Gary kama mtu wake bora" Leo katika uchunguzi wa mauti ya Gary Speed ​​yamethibitisha alionekana kunyongwa katika nyumba anayoishi yeye na mke wake, hakika ni habari za kushangaza.

Picha za mwisho wa uhai wake... Gary Speed ​alikutana na mashabiki katika studio BBC mjini Salford, Manchester.

Mashabiki wengi walijivunia kupiga picha alongside Wales boss Gary Speed

Hayden Evans wakala wa Gary Speed.
"Kila mtu amekuwa akiuliza swali moja na hakuna mtu yeyote mwenye jibu kwani sote tuko katika mshtuko, Jambo moja naweza kusema kuwa familia na mimi kama mmoja wa rafiki zake wa karibu kabisa bila kukanusha ni kwamba hapakuwa na dalili ya matatizo yoyote na kamwe imekuwa.."

"Kwa nini hakuweza kunipigia simu kwa ajili ya kuzungumza kile kilichokuwa kikimtatiza kwa ule muda kabla hajafanya aliyoyafanya?"

"Nilikuwa pamoja naye siku ya Jumamosi tukishuhudia mchezo wa Stoke na mwisho wa siku tukaweka mikakati wiki ijayo"

"Alikuwa anakuja nyumbani kwangu pamoja na mke wake tunakaa pamoja katika nyumba yangu, Tukienda dinners mbalimbali.. Tuliondoka studio, tukashikana mkono na kusema, 'See you next weekend.' Unfortunately I won't."


Shabiki wa Bolton, moja ya timu alizopata kuchezea... akiwa amepiga magoti kutoa heshima za mwisho mbele ya maua na jezi za Gary Speed.

Sheffield ... team shirts outside the Blades' Bramall Lane.
Naye mchezaji maarufu wa zamani wa New Castlle United Alan Shearer amesema kuwa hakuna mtu anayeweza kuelezea dhiki yake iliyompata moyoni juu ya kifo cha rafiki yake huyo. Shearer said: "I played against him many times, but when Kenny Dalglish signed him for Newcastle straight away we struck up a relationship. You're bound to have arguments along the way in football — but no one ever did with Gary.

KUANZIA SASA JERRY MURO YUKO HURU

Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari leo baada ya kuachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.(Picha na Issa Michuzi)
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijijini Dar es Salaam imemwachia huru na kuwafutia mashtaka aliyekuwa 'JEMBE' Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jerry Muro pamoja na washtakiwa wenzake wawili ambao ni Edmund Kapama na Deogratius Mgasa waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya tsh.10 milioni.