ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 9, 2011

MAPICHA YETU.... BLOGUNI'

Flowerz kutoka chuo cha St.Agustin katika pozZ la ki-face book.

Anaza pic pande hii'::: smaaaaili'

Dj Ally coco, Z-anto na mdafada pale kati, sijui ni shemajiii?

One pick at ze-ples Mie, Mansulee na Kabago.

GirlZ at easy....

Shabiki wa chama la ukweli Bwawa la maini naye akijimix kapetini.

Sshh!

MadoctaZ toka Bugando Braza Ngwasuma na mie.

Sehemu nzuri, watu wazuri, muziki mzuri ni STONE CLUB 'Mwanza bwana'.

Infwakiti' We be clubin at the place away with the gloom, ze grass gently waves and after all the birds peacefully fall to sleep.

Friday, April 8, 2011

**RED CAPET STONE CLUB" **

Usiku wa leo ni Red Capet ndani ya shimo la maraha ya asali na utamu STONE CLUB MWANZA aka 'Ze-jiwe': Vaa upendeze tupia ile ya MWISHO kabatini tukapige mapicha kwa ma-face book, matwitter na mablogu...Hallla!"

REAL MADRID WANYAKUWA KOMBE SERENGETI FIESTA BONANZA 2011 DAR.

Timu ya soka ya mashabiki wa Real madrid ya jijini Dar es salaam ndiyo imeibuka kuwa mshindi katika ligi ya Tamasha la Fiesta Soka Bonanza iliyofanyika kwenye uwanja wa Leaders jana hivyo kunyakuwa kombe na zawadi ya Fedha taslimu shilingi milioni moja. Timu hiyo imepata ushindi huo mara baada ya kuingia fainali na hatimaye kuishinda timu ya mashabiki wa Chelsea ambao nao wametoka na zawadi kama washindi wa pili ya shilingi laki tano.

RABSHA NAZO SEHEMU YA MICHEZO. 'Siunajuwa hawa ni mashabiki wa timu gani na gani?' Katika hatua ya nusu fainali Chelsea waliwaondosha Manchester United nao Real wakawagagadua Ac milan.

Mashindano hayo yataendelea tena katika mikoa mbalimbali hapa nchini yakishirikisha mashabiki wa mikoa husika kwa timu tajwa katika mashindano ambazo ni Man United, Liverpool, Chelsea, Real madrid, Bacelona, Inter Milan, Ac Milan na Alsenal.


Masanja mkandamizaji wa Ze Orijino Komedi katika pozi naye Babuu wa Kitaa toka Ze-supa Brand Clouds Media viwanjani hapo kama mashuhuda kwa yaliyojiri.

MASHABIKI MWANZA PASHENI MISULI...INSHU YAJA..

MASANJA WA ZE ORIJINO KOMEDI KUWA MC, NAYE 20% KUMWAGA BURUDANI MISS KILIMANJARO 2011

Shindano la kumsaka mnyange wa Kilimanjaro 2011 linategemewa kuanza hivi karibuni baada ya waandaji wa shindano hilo kudai kuwa sehemu kubwa ya maandalizi imeanza kukamilika ikiwa na pamoja kuwakusanya warembo kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya mazoezi (catwalk).

Msemaji wa shindano hilo Bw.Methuselah Magese amesema kuwa yeye na mundaji mkuu wa shindano hilo Jaquekline Chuwa tayari wako katika mchakato mnene kuhakikisha miss Tanzania wa mwaka huu anatokea mkoani Kilimanjaro.

Shindano la miss Kilimanjaro litafanyika june 11 juni katika hoteli nya Salsanero iliyoko Shant town mjini Moshi ambapo mchekeshaji masanja toka kundi la Ze Komedi Orijino atakuwa ndiye mc wa siku hiyo wakati msanii 20% na wengine wengi wataburudisha vya kutosha.

Miss kilimanjaro 2011 imedhaminiwa na Vodacom, Redds, Africa sana pub,Rafiki min super market, Excutive solution, Bamm solution na www.uniqueentertz.blogspot.com.

"Tunawaomba warembo wanaojiamini kuwa wao ni warembo na wenye ari ya kuwa vinara wa sanaa ya urembo wajitokeze kuwania taji hilo ambalo litakuwa na ushabiki wa aina yake kwani tunategemea kutoa warembo bomba ambao watatoa changamoto kwa vitongoji na kanda zingine" alisema magese.

Thursday, April 7, 2011

MOTO WAZUKA KIWANDA CHA MAKASHA (MABOYA) YA KUSAFIRISHIA SAMAKI MWANZA

Moto uliozuka leo majira ya saa saba mchana kwenye kiwanda cha Falcon kilichopo Igogo Wilayani Nyamagana Jijini Mwanza umeunguza bidhaa na baadhi ya mitambo hivyo kusababisha hasara kubwa kwa wamiliki wake.Ikiwa ni mara ya pili kwa kiwanda hicho cha kuzalisha makasha ya kuhifadhia samaki kuungua tangu moto uliotokea mwezi Mei 26 mwaka jana na kufanyiwa ukarabati ambao bado ulikuwa naendelea, safari hii kiwanda hicho kimeungua na kusababisha hasara kubwa ya malighafi ambayo tayari ilikuwa imetengenezwa na kuwa bidhaa.

Moto huo umeunguza baadhi ya mashine mpya za kiwanda hicho sambamba na makasha mengi yaliyokuwa yakisubiri kupelekwa viwanda vingine vilivyopo jijini Mwanza, Mara na Kagera kupakiwa minofu ya samaki kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi.

Wafanyakazi wa kiwanda hicho waliozungumza na mwandishi wa habari waliofika katika tukio hilo kwa sharti la kusitiriwa majina yao wamesema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme kwa mitambo iliyosababisha cheche za moto zilizoruka hadi kwenye makasha ya maboya ambayo tayari yalikuwa yamezalishwa.

Mashuhuda hao wameongeza kuwa kuwa moto huo baada ya kudaka maboya ulishika kasi na kunasa katika sehemu nyinginezo kiwandani hapo zikiwemo mashine na vifaa vingine kabla ya kikosi cha zima moto kufika na kuudhibiti moto huo.

Biju Zacharia (wa3 kutoka kulia) ambaye ni meneja uzalishaji wa kiwanda hicho amesema kuwa bidhaa nyingi zizalishwazo kiwandani hapo zimeungua na pia moto huo uleta hasara kubwa ambayo bado haijafahamika.

KUMBUKUMBU


*******************KUMBUKUMBU YA MASUBO********************
Familia ya marehemu Fidelis Michael Masubo inapenda kuwakaribisha ndugu, Jamaa na Marafiki wote kwenye misa fupi ya kumbukumbu ya kutimiza miaka miwili Tangu atutoke Baba yetu mpendwa Fidelis Michael Masubo.


Misa itafanyika Nyumbani kwake Myakato Buzuruga siku ya ijumaa (kesho) Tarehe 08/04/2011 kuanzia saa 1:00 usiku, Hii ikiwa na lengo la kuwapa nafasi waumini wa Kanisa Katiliki kuhudhuria kwanza misa ya njia ya msalaba.

ENYI NDUGU NA MARAFIKI Njooni tujumuike PAMOJA katika sala.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
*****************************AMEN******************************

SERENGETI FIESTA SOCCER BONANZA YARINDIMA VIWANJA VYA LEADERS CLUB LEO.

Wakiongozwa na jeshi la Polisi nchini mashabiki wa vilabu mbalimbali vya Ulaya jijini Dar es salaam hii leo wameandama hadi viwanja vya Leaders Club kwa ajili michezo ya ufunguzi wa Tamasha la Fiesta 2011 kupitia soka ambapo mashabiki hao waliunda timu zao ambazo zilizotengenezewa ligi ya inayoendelea sasa viwanjani hapo. Mashabiki wa Mwanza na mikoa mingine jiandaeni... Taarifa zaidi sikiliza Clouds FM. Time hii vipute vikiendelea kama kawa.

REAL MADRID Dar.

LIVERPOOL Dar.

AC MILAN Dar.

BARCELONA Dar

ARSENAL Dar

CHELSEA Dar.

MAN U Dar.

KIKOSI INTER MILAN Dar.

Picha zote na Michuzi jr (JIACHIE)

MATEMBEZI YA KUMUENZI RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR YAFANYIKA LEO. NAMI NA UJUMBE''''

Picha na Ramadhan Othman Abdalla.
Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya taifa CCM,Dk Ali Mohamed Shein,akipokea matembezi ya kumbu kumbu ya miaka 39 ya kumuenzi muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar,hayati Abeid Amani Karume,katika viwanja vya CCM Afisi kuu Kisiwandui leo.

Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya taifa CCM,Dk Ali Mohamed Shein huku wakionesha bango lenye Picha na ujumbe wa kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar,wakati wa mapokezi ya matembezi ya kumuenzi rais huyo yaliyopokele wa na Rais wa Zanzibar katika viwanja vya CCM Afisi kuu Kisiwandui leo.

Leo tunapoadhimisha kumbukumbu ya mapinduzi ya zanzibar ya tarehe 12 january 1964 kuna haja kuikumbusha serikali kuwa kuna jambo moja muhimu inalopaswa kulizingatia katika kutunza kumbukumbu na kukilinda kizazi chake nalo ni Kuweka utaratibu utakaowawezesha vijana wake wa sasa kupata elimu ya kujua historia ya matukio muhimu ya taifa letu la Tanzania. Kwani ndani ya zama hizi kumekuwa na mkanganyiko katika masuala mbalimbali ya kijamii na kisiasa kutokana na kizazi cha sasa kuuweka kando 'wakati uliopita' na kuzingatia 'wakati uliopo' na 'wakati ujao'.

KARUME DAY OYEEE
@g.sengo

Tuesday, April 5, 2011

ROLI LA MAFUTA LATUMIKA KUSAFIRISHA SHEHENA YA BANGI : POLISI MWANZA WAWATIA NGUVUNI WATUHUMIWA WATATU.

ASKARI KANZU WAKISHUSHA SHEHENA HIZO ZA BANGI.
Ni gari la kusafirisha mafuta aina ya Scania lenye namba za usajiri T263 BLL lililokamatwa na Jeshi la polisi mkoani Mwanza hii leo mara baada ya ukaguzi kufanyika na hatimaye kushikiliwa eneo la beria ya wilayani Magu mkoani Mwanza.

BANGI.
Awali katika ukaguzi huo kwenye beria ya Magu jeshi hilo liligundua shehena ya madawa ya kulevya hayo aina ya bangi kwa mzigo uliopakiwa juu ya tanki la mafuta ambao ulikamatwa na kupelekwa moja kwa moja kituo kikuu cha Polisi Mwanza.

"MURAaa RINGINE HIRI HAPA.!"
Lakini kituoni hapo wakati ushushaji ukiendelea, katika shughuli za upekuzi zaidi moja kati ya makachero wa jeshi la polisi aligundua shehena nyingine kubwa ya bangi iliyokuwa imehifadhiwa sehemu ya nyuma, chini ya tanki hilo la mafuta yenye upenyo mithili ya kisanduku cha kuhifadhia mizigo.

Ndipo ushushaji wa shehena hiyo ukafanyika huku ukiwapa shida washushaji kwani ilikuwa imeshindiliwa kiuakika mithili ya robota la pamba linavyshindiliwa.

DEREVA WA GARI HILO BASHIRI WAZIRI.
Inadaiwa kuwa Dereva wa gari hilo Bashiri Waziri alijaribu kudanganya kuwa ndiye aliyetoa taarifa kufanikisha muhusika wa shehena hiyo na zigo lake kukamatwa na jeshi hilo. Akisimulia kwamba eti' mara baada ya kupakia mzigo huo kutoka kwa mtuhumiwa asijue kama amebeba madawa haramu ya kulevya huku mmiliki wa mali hiyo akimwambia kuwa shehena hizo niza mbogamboga za majani anazosafirisha kuelekea jijini Dare s salaam, aliutilia mashaka baadaye njiani wakati wakipumzika kwenye baadhi ya vituo kwa kuhisi harufu kama ya bangi na ndipo alipo tafuta chemba na kuwapigia askari wa kituo cha beria kinachofata kuingia jijini Mwanza eneo la Magu ambapo askari walifanya upekuzi na hatimaye kubaini ukweli. MMMh!

MMILIKI WA ZIGO HILO MGESI ANTONY (41).
Katika tapatapa nae mtuhumiwa mmiliki wa zigo hilo haramu Mgesi Antony (41) kabila mkurya ambaye ni mkulima mkazi wa wilaya ya Tarime mkoani Mara alitamka dhahiri kwenye beria mahala alipokamatwa kuwa yuko tayari kutoa rushwa ya shilingi milioni moja kwa askari hao ili mzigo wake upate ruksa kuendelea na safari , askari hao waligoma na hatimaye kumfikisha kituo kikuu cha polisi Mwanza.ZOEZI LA UPAKUAJI.

TBC AKIWAKILISHA.
Bangi hiyo ilikuwa ikisafirishwa kuelekea jijini Dar es salaam ilikuwa ikitoka eneo la Lamadi mkoani Mara eneo linalosadikika kuwa maarufu kwa biashara hiyo haramu tena wakazi wake wakichukulia poa’ yaani kama biashara nyingine za kawaida. Polisi inaendelea kuwashikilia watuhumiwa wote watatu akiwemo utingo wa roli hilo kwa ushahidi zaidi.

HONGERA DADA PILLY KWA KUTULETEA BABY GIRL.

Hongera da-Pilly Mgori kwa kujifungua salama siku ya jumamosi na kutuletea Baby Girl.

Kama ilivyoada kwa waafrika na tamaduni zetu mie na swahiba wangu Humphrey Simon siku ya jana tulidhuru hospitali ya Mwananchi Mwanza kumjulia hali, Alhamdulilah mambo yalikuwa swafiZ.


Humprey Simon wa kitengo cha masoko Clouds Mwanza akipata baraka za mtoto wa sis Pilly.

Nami pia na totoo.

Monday, April 4, 2011

ZIARA YA RAIS WA SOMALIA SHARIF SHEIKH AHMED NCHINI TANZANIA YAAHIRISHWA.

SHARIF SHEIKH AHMED.
Ziara iliyokuwa ifanywe na Rais wa Somalia SHARIF SHEIKH AHMED, nchini Tanzania kuanzia tarehe 6 hadi tarehe 7, 04,2011 Imeahirishwa mpaka pale itakapotangazwa tena.

IMETOLEWA NA ISHENGOMA
AFISA HABARI MWANDAMIZI.

20% AZIANIKA TUZO ZAKE KATIKATI YA SHOW YA KUFUFUKA MTU YA MAPACHA WATATU.

Mwanamuziki 20% amefanya makamuzi matata sana na yakuvutia katika show wakati iliyofanyika jana usiku pale alipojumuika na Bendi ya Mapacha Watatu ndani ya Ukumbi wa Mzalendo Pub.

Mwendo kusikilizana na kugawa maladha ya ukweli palekati ni 20% akiwa na Josee Mara wa Mapacha Watatu.

Producer producer kweli nikimaanisha mwanamuziki ni Man Water or Man Maji akizicharaza vilivyo Tumba wakati 20% akitumbuiza.

Tuzo nilizo nyakuwa mwanenu ni hizi hapa akiambatana na kampani yake kuzianika tuzo za Kili 2011.

Kama ni mwandiko darasani basi huu ni mcharazo, ni pale patamu penye sebene'na Mapacha Watatu.

Hawa ndiyomapacha watatu kutoka shoto Kharid Chokoraa, Jose Mara na Kalala Junior wakiimba moja ya masongi pendwa ya bendi yao.
PICHA ZOTE NA HABARI HISANI YA mtaakwamtaa.