ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 1, 2011

BROTHER'S & SISTER'S STONE CLUB SNDO' PENYEWE

Wadau EEEeeH! Mara baada ya uchovu wa safari kutoka kwa Babu Njooni tujumuike pamoja leo tule bata, tugonge mojamoja-mbilimbili ndani ya kiwanja chetu : Ni pare-pare STONE CLUB Mwanza aka ZE-JIWE, Mwanza will be burning Mzeeeyaah!
!!USKOSE!!

WAMESHA KIRAMBA!

HII NDIYO hali halisi....Ni eneo linalokulazimu kupunguza mwendo kasi na kusimama kabisa kisha ukaingia kipitashoto kilicho katikati ya ROCK CITY.... lakini sasa..! SIWAMEKIRAMBA.

MKALI NANI KATI BONGO FLEVA V/S MWANZA STAR KUJULIKANA KESHO CCM KIRUMBA.

Kutoka kushoto H.baba, Inspector Haroon, Kabago, Jebby, Ben Kinyaiya, Suma G. na Mansulee.

Ule mtanange wa kukata na shoka unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka kanda ya ziwa baina ya timu ya Bongo Fleva na Watangazaji & Madj wa jiji la Mwanza aka 'Mwanza stars' ndiyo hivyoo umebakiza saa kadhaa upate kuchukuwa nafasi, nazungumzia kesho jumamosi katika dimba la CCM kirumba.

Tayari baadhi ya wachezaji wa timu ya Bongo Fleva wamekwisha wasili jijini Mwanza kwaajili ya mpambano huo wakishiriki hatua kadhaa za matayarisho ya kipute hicho huku wengine wakitaraji kutua usiku wa leo na Precision air Pichani kutoka kushoto ni H.Baba (jembe la Bongo fleva) Suma (Bf) Philbert Kabago (kapten wa Mwanza stars) Omari (mratibu wa pambano) na G.Sengo (Mzs')baada ya mahojiano Radio Passion mchana wa leo.

WAZIRI WA LIBYA AHOJIWA UINGEREZA

Waziri wa mambo ya nje wa Libya Mousaa Koussa amekuwa akihojiwa na maafisa baada ya kuwasili Uingereza bila kutarajiwa siku ya Jumatano.Alitokea Tunisia. Ofisi ya Uingereza ya mambo ya nje ilisema "hakuwa na nia tena" ya kufanya kazi na Kanali Gaddafi.

Hata hivyo msemaji wa Libya alikana kwamba Bw Koussa ameasi na kwamba alikuwa katika safari ya kidiplomasia. Kuwasili kwake Uingereza kumefanyika huku waasi wa Libya wakiwa wamerudi nyuma kwenye miji iliyotekwa hivi karibuni katika pwani ya mashariki.

Kurudi nyuma kwa waasi kulitokana na mapigano makali baina ya Brega na Ajdabiya siku ya Alhamis. Awali waasi hao walishapoteza bandari muhimu ya mafuta ya Ras Lanuf na mji mwengine ulio karibu wa Bin Jawad.

Upande wa magharibi, mji ulioshikiliwa na waasi wa Misrata bado unaripotiwa kushambuliwa na majeshi ya wanaomtii Kanali Gaddafi.


KWA HISANI YA bbc swahili.

Thursday, March 31, 2011

MABANGOzz!!

Fisi akiwa hakimu...

Acha ropo ropo jombaa..Fanya kazi...

Muweke Mungu mbele.

MCHEZO NA BONGO FLEVA FC=VSS SECURITY KWA KUSHIRIKIANA NA STONE CLUB WAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA SOKA YA MADJ NA WATANGAZAJI MWANZA.

Timu ya soka ya Bongo Fleva ambayo hivi karibuni iliwaangusha wenzao wa Bongo Movie kwa kuwacharaza bakora mbili kavu Siku ya Jumamosi inategemea kushuka dimbani Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kukiputa na timu ya Watangazaji na MaDJ wa Mwanza.MENEJA UWEZESHAJI WA VSS MR.MAX (KUSHOTO) AKIMKABIDHI VIFAA MENEJA MCHEZAJI WA TIMU YA WATANGAZAJI NA MADJ MWANZA DJ ALLY COCO, PEMBENI YAKE NI KAPTENI WA TIMU HIYO PHILBERT KABAGO.
Katika kujiandaa na mchezo huo Kampuni ya Ulinzi jijini Mwanza ambayo pia ni moja kati ya wadhamini wa Blogu hii VSS Security Group kwa kushirikiana na club maarufu jijini Mwanza STONE CLUB jana jioni wamemwaga Ma-Full seti ya vifaa vya michezo Jezi jozi mbili, Shin guard, Sox na Viatu kwa timu ya Watangazaji na MaDJ wa Mwanza.

ALLY COCO (SHOTO) NA KABAGO MBELE YA UZI MPYA.
Kiingilio kwa mchezo huo ni shilingi 2,000/= mzunguko na 3,000/= jukwaa kuu. Burudani ya muziki wa bongo fleva kutawala jukwaani kuanzia saa 6 mchana kabla ya mchezo.

Timu ya Watangazaji na MaDJ ikijifua katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kujiandaa na mchezo baina yake na timu ya Bongo Fleva Fc Jumamosi hii.

M 2tha P ambaye ni msemaji wa Bongo Fleva FC amesema kwamba timu hiyo itakuwa jijini Mwanza kwa mechi moja na timu itaambatana na nyota wake ili kulipendezesha pambano lao. Wachezaji ambao watasafiri na timu ni pamoja na Ngwear, Ben Kinyaiya, H-Baba, Soggy Doggy, Suma G, Richie One, Insepecta Haroun na Q Jay. Wengine ni KR Mullah, Z Anto, Godi Mwokozi, Kalapina, Mansu Li na yeye mwenyewe M 2tha P.

USIKOSE JUMAMOSI HII....CCM KIRUMBA

MBUNGE WA CHADEMA ILEMELA MWANZA ATIMIZA AHADI YAKE NDANI YA SIKU 90 ZA UONGOZI WAKE. MH. SUGU ALAZIMISHWA KUCHANA SHANGWE ZALIPUKA!!!

MBUNGE wa Jimbo la Ilemela, mkoani hapa, Mh. Highness Samson Kiwia, amewataka wananchi kutunza vitendea kazi mbalimbali vinavyotolewa na wafadhiri, serikali na taasisi mbali mbali ili viweze kutumika kwa muda mrefu kwa manufaa yao.MH. MBUNGE (KULIA) AKIKABIDHI MSAADA HUO.
Alisema hayo wakati alipokuwa akikabidhi gari la kubebea wagonjwa aina ya Nissan Patrol lenye thamani ya shs.millioni 32 katika hafla fupi iliyofanyika katika Zahanati ya Karume, iliyopo katika kata ya Bugogwa wilayani Ilemela.

Katika kampeni za uchaguzi ambao ulimalizika mwishoni mwaka jana, aliwahaidi wananchi katika jimbo lake kuwa atawasaidia gari la kubeba wagonjwa ambalo litawasaidia wananchi kuwasafirisha hadi katika hospitali zingine na baadhi yao kuwatoa majumbani kwao hadi katika zahanati hiyo ahadi ambayo ameitekeleza ndani ya siku 90 kama alivyoahidi.

WANANCHI WAKITATHMINI GARI LAO.
Mhe.Kiwia ametoa ahadi nyingine kuwajengea wananchi wa kata ya Bugogwa, kituo cha polisi na kumuagiza Diwani wa Kata ya Bugogwa, Swila Dede Swila ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo, kata ya Bugogwa kusimamia ujenzi wa kituo hicho ambacho kitaanza kujengwa muda wowote kuanzia sasa na ujenzi wake kukamilika ndani ya siku 90.

Mganga Mfawidhi katika Zahanati ya Karume, Bernard Straton, amemshukuru mbunge kwa msaada huo na kuongeza kuwa gari hilo ni msaada mkubwa kwa wananchi wa kata ya Bugogwa na kumuomba mbunge huyo kutoa ufadhiri wa aina nyingine pale ambapo utahitajika katika zahanati hiyo.

MH. AKICHANA' MISTARI.
Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi al maarufu kwa jina la Mr. sugu alikabiliwa na wakati mgumu baada ya kulazimishwa kuimba jukwaani pasipo kupanga, hiyo ni mara baada ya kuhutubia. "Tunataka UCHANE" , "CHANA MISTARI NDIYO UKAE" sauti zilisikika! Bila hiyana akawapa mistari ya kutosha ya wimbo - Wananiita sugu! ......Akashangiliwa ile mbaya na mamia yaliyohudhuria makabidhiano hayo.

Ametoa maelekezo kwa watendaji ngazi ya kata kuwa na ushirikiano wa karibu katika kukamilisha mipango mbalimbali aliyoiweka ikiwa ni pamoja na ujenzi huo wa kituo cha polisi, kufanya kazi bila kutegeana na kusema kuwa suala la ulinzi ni haki ya kila mwananchi na hivyo kukamilika kwa kituo hicho itakuwa ni mojawapo ya kuwahakikishia usalama wao na mali zao.

MBUNGE HIGHNESS AKITIA SAINI KITABU CHA MAKABIDHIANO.
Mbali na hayo, mh. Mbunge pia ameahidi kuendeleza miradi mingine ikiwemo ukarabati wa barabara, usambazaji wa maji safi kuwa itasimamiwa kikamilifu lengo likiwa ni kuleta maendeleo kwa wananchi wa kata ya Bugogwa na jimbo la Ilemela kwa ujumla.

Wednesday, March 30, 2011

KWENDA LOLIONDO KWA BABU SASA TAMBARARE, NJIA YA NDABAKA YAPIGWA MARUFUKU - KIKOMBE KINGINE CHAIBUKA MAGU

Katika kudhibiti usalama, hali mbaya ya huduma za afya, malazi, chakula, maji na huduma nyingine kwa mahitaji ya mwanadamu Serikali mkoani mwanza kupitia kamati yake ya ulinzi na usalama leo imetoa taarifa kwa vyombo vya habari jinsi ilivyo jipanga kuhakikisha watu wake wanaosafiri kuelekea kijiji cha Samunge wilaya ya Ngorongoro kupata tiba wanapata tiba bila usumbufu na hatimaye kurejea salama.Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema kuwa katika kipindi cha tiba ya babu wa loliondo ofisi yake imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ikiwa ni pamoja na watu kuachwa njiani bila msaada wowote, kutofikishwa kwa mchungaji kupata tiba kutokana na ubovu wa vyombo vya usafiri na baadhi ya watu kupoteza ndugu zao bila taarifa.

Kupitia sababu hizo na nyingine nyingi za kiusalama na kepuka mfumuko wa bei ya vyakula kijijini na nauli kwa vyombo vya usafiri Kamati yake imekuja na utaratibu mpya utakaofuatwa na watu wote ili kupunguza kadhia iliyopo na msongamano huo.

Aidha bwana Abbas Kandoro amesema kuwa serikali imeamua kuunda vituo vya kanda vilivyopewa majukumu ya
-Ukaguzi wa magari ambapo malori na magari ya wazi yamepigwa marufuku kuelekea Samunge.
-Utoaji wa namba za magari kwa kila kanda kuwa na rangi yake maalum, Kanda ya ziwa - Nyekundu, Kanda ya Kaskazini - Njano na Kanda ya Kati - Kijani.
-Ukaguzi wa wasafiri kutoka nje ya nchi
-Utoaji wa leseni za muda/ vibali maalum
-Kuangalia wagonjwa mahututi
-Kutolewa kwa matibabu ya dharura
-Usalama wa vituo na
-Kupanga muda wa kuondoka


Amezitaja kanda tatu zilizoundwa za uthibiti wa usafirishaji wa abiria kuelekea Loliondo ambazo ni Kanda ya ziwa vituo vikiwa Musoma , Bunda, Mugumu na Loliondo/ Wasso,huku njia ya Ndabaga ikipigwa marufuku, Kanda ya Kaskazini ambayo itahusisha mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Zanzibar na nchi jirani huku vituo vilichoainishwa vikitajwa kuwa ni Arusha mjini – viwanja vya NMC, Loliondo na Mto wa Mbu.

Wadau wa vyombo vya usafiri katika mkutano huo.
Kanda nyingine iliyotajwa ni Kanda ya Kati ikihusisha mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Manyara na Nyanda za juu kusini nacho kituo kikiainishwa kuwa ni babati.

Taarifa hiyo imewataja wasimamizi wakuu wa kanda kwa utawala kuwa watakuwa Wakuu wa mikoa ile hali utekelezaji utasimamiwa na RPC, RIO, RMO, JWTZ, TAKUKURU, RSO, SUMATRA, TRA na TANROADS.

Wakati huo huo taarifa kutoka kijiji cha Bulima katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza zinasema kuwa kikombe kingine kimeibuliwa na mtu anayejiita SHANGAZI (Marieta Charles) ambaye ameibuka akitoa tiba ya dawa ya miti shamba yakunywa vikombe viwili kwa gharama ya shilingi 1000.


USAFIRI TOKA ARUSHA KWENDA LOLIONDO KWA BABU PEMBEZONI MWA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID.
Serikali ilisitisha safari kwenda kijijini Samunge kwa muda wa wiki moja kuanzia jumamosi ya tarehe 26/03/2011 hadi tarehe 01/04/2011 kwa magari yote hii ikiwa ni pamoja na magari ya serikali na viongozi wa aina zote, usafiri kwa njia ya ndege na Helkopta, sababu kuu zikitajwa kuwa ni hali tete za Afya, mazingira na huduma muhimu.

Tuesday, March 29, 2011

KOMENTI ZA WADAU MITANDAONI KUHUSU DAWA YA BABU ...

Mara baada ya serikali kutoa tamko la kuridhishwa kwake na dawa inayotolewa na mchungaji Ambakile Masapila wa kijiji cha Samunge Loliondo ikisema haina madhara yoyote kwa matumizi ya binadamu, watu kupitia mitandao mbalimbali wamekuwa wakidondosha maoni yao.. ->#67 maishaduniangumu JR 2011-03-29 16:06
HII NI NEEMA,PATA DOSE MOJA NENDA SUBIRI SIKU KADHAA, PIMA ILI UJUWE HALI YAKO UPO KAMA ZAMANI AU LA....
Quote

->#65 GEOFREY 2011-03-29 15:13
KUNA TETESI NIMESIKIA OSAMA AMEPATA KIKOMBE KWA BABU. NAOMBA WADAU MNITHIBITISHIE.
Quote

->#64 MASHILINGI 2011-03-29 15:09
WE KIPARA ACHA UJUAJI MWINGI WA KUZUNGUKA SEHEMU MOJA. NI WAGANGA WANGAPI WALIOPO TZ NA AMBAO WAMEKUWA WAKITANGAZA KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUWA WANATIBU MAGONJWA SUGU. SASA CHA KUSHANGAZA BABU HAJAWAHI MTANGAZIA MTU YEYOTE ISIPOKUWA WE UNAYEPONYWA NDO UNAENDA KUTANGAZA. ACHA TABIA ZA AKINA ROSTAM NA KAKOBE NJOO UPATE KIKOMBE UPONE.
Quote

->#61 kipara 2011-03-29 14:57
Hapa pana utata ambao haujatatuliwa. Utata wenyewe ni je! hii dawa inatibu kweli? tuacheni hadithi za vichochoroni na tupeni ukweli wa kitaaluma kuhusu majaribio ya dawa hizi kabla ya kikombe na baada ya kunyweshwa hicho kikombe. Kwa mantiki yangu inaonekana hapa upo kamchezo ambao unanufaisha wajanja wachache na mwisho wa mchezo tutakuja kugundua kwamba wengi wametajarika na huu kamchezo. Tamko la serikali kwamba dawa haina madhara bado haijajibu hoja.Inawezekana wako wanahisa katika hii scheme wanamikono mirefu hadi kuwashawishi watoaji wa maelezo ya kuipa uhalali hii dawa hewa.
Quote
->#58 jenisia 2011-03-29 14:19
watu wamepona magonjwa sugu, hasa vigogo ndio maana serikali inamuunga mkono. hakuna cha siasa wala CCM. Babu kaza mkono kugawa Kikombe!
Quote

->#57 Deogratius 2011-03-29 14:19
Mbona imani zenu ndogo hivi kweli hamjiulizi watu wote hao wanaweza kwenda kwenye hamna? pole sana.. Mungu wetu wasaidie hao watambue ukweli maana hata ulivyo mtuma YESU wengi walimpinga ktk mambo na uponyaji aliokua akiufanya, mpaka leo hii bado kuna Wayahudi hawamtambui!!!! Vivyo hivyohata kwa kizazi hiki, nawaambia nendeni mkapate tiba kama mimi, sitaki kueleza zaidi ya kuwa watu WANAPONA na nimepona hiyo dawa ni ya ajabu 'it's beyond our understanding' pia kumbukeni kua kizuri hakidumu kama una tatizo please nenda ukitaka kudadisi sana huna matatizo na kama unayo basi utapitwa mbarikiwe sana >AMINA
Quote

#54 Ndazu 2011-03-29 13:47
Huyo mzee ameweka wazi kuwa lazima uwe na imani na bila shaka ni imani ya Mungu sasa lazima tujue kuwa kuna tofauti ktk Mungu tunayemuamini wengine wana watatu, wengine mizimu wengine wanaabudu mashetani na WENGINE WANAMWAMINI MUNGU MMOJA TU HAKUZAA WALA KUZALIWA AMBAYE KILA KITU KINAMTEGEMEA YEYE NA WALA HANA KINACHOFANANA NAYE sasa wale wanaokunywa KKKT (Kunywa kikombe Kimoja TU) wajiulize wao wana muamini mungu yupi na Babu anamuamini mungu yupi hapo watapata majibu TCHAO
Quote

POZI LA KIKATUNI......

NANI KATISHA?
Kutoka kushoto>Bonge (clouds), Anord Kayanda (clouds), Milard Ayo (clouds) na Joti (orijino komedi TBC1).

JUU KWA JUU JIJI LA DAR ES SALAAM.

Kutokana na mabadiliko ya ujenzi katika fukwe za bahari ya hindi, baadhi ya mito kukauka na kufutika kabisa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, michoro mipya ya barabara na ujenzi wake tofauti na miaka ya 1970 na 80, Jamaa mmoja niliyekaribu naye angani hapa anahoji kwambaa.."Kwanini wataalam wetu wa kupanga miji, wasilione hili na kuchora ramani mpya ya Jiji la Dar es Salaam?"
A

B

C

D

E

FSehemu ya jiji kwa ukaribu kidooogo.

Monday, March 28, 2011

PICHA ZAIDI NDANI YA RED CAPET YA KILI AWARDS 2011

Ma-mc walioongoza shughuli hiyo.

Idadi kubwa ya watu ninaokutana nao kila mmoja wakizungumzia inshu nzima hawakosi kuitaja burudani hii iliyoporomoshwa na Ally Kiba, Banana Zorro na Diamond.

Utu Uzima Dawa- Ally Kiba, Said Mabela, Banana Zorro na Diamond

Dina Marious akimtangaza mshindi tuzo ya Rapa bora muziki wa Dansi.

Kwaheshima na kuwaombea waliofariki dunia kwenye ajali ya 5star morden taarab iliyotokea hivi karibuni Umma uliokuwemo ukumbini hapo ulisimama kwa dakika moja.

All star.

'Ze Kruu Inza Hausi' kutoka kushoto Dataz, Reuben Ndege, Babuu wa Kitaa na Sebastian Maganga.

Ni burudani iliyowalazimisha watoka mapema kubakia ukumbini hakika Waandaaji hawakukosea kuiweka burudani hii mwisho kabisaaaa, Unajua kwanini wanaitwa Mapacha Watatu?

Nje ya ukumbi kabla ya shughuli kutoka kushoto Mie na mkali wa bongo fleva nchini Chege na mratibu wa THT Hamza.

Sunday, March 27, 2011

SHANGWE ZALIPUKA WAKATI 20% AKING'ARA TUZO ZA KILIMANJARO 2011: MAPINDUZI YAONEKANA

Tuzo zenye hadhi ya juu Afrika Mashariki zenye jina 'Tanzania Kilimanjaro music Award' hatimaye zimefanyika ndani ya Diamond jubilee jijini Dar es salaam huku msanii wa muziki wa Bongo Fleva 20%aking'ara kwa kuondoka na tuzo 5 ndani ya vipengere tofauti. Producer Man Walter alipokea tuzo zote kwa niaba ya 20%

20% AMENYAKUWA TU HIZI:
Msanii bora wa kiume,
Mwimbaji bora wa kiume,
Wimbo bora wa mwaka- Tamaa mbaya.
Mtunzi bora wa nyimbo,
Wimbo bora wa Afro pop- Tamaa mbaya.


Barnaba toka THT hakika alistahili kuitwaa tuzo hii Wimbo bora wa zook/rhumba kupitia wimbo Nabembelezwa: Naaaam - ilimilikishwa huku akishangiliwa na hadhira iliyo kuwa eneo la tukio.

Mwanamuziki mkongwe kutoka Msondo ngoma music band Said Mabela akitoa zake shukurani mara baada ya kutunukiwa Tuzo ya Hall Of Fame mie naiita Tuzo ya Uvumilivu, kwa ufupi mcharazaji huyu wa gitaa la solo hajawahi hama bendi hiyo tangu ajiunge nayo, yaani bendi inabadili majina yeye yupo tuu mpaka leo.

Kwake binafsi wakati akizungumza mara baada ya kupokea tuzo ya Wimbo bora wa asili wa Tanzania, Mpoki wa Orijino Komedi alisema "Kwangu mimi kupokea tuzo hii ni maajabu ndani ya maisha yangu, kwani kupata tuzo hii kwangu mie ni sawa na mwanamke asiye na mimba kuzaa..."

Joe Makini akifanya mahojiano na Swahiba Antonio Nugaz wa clouds Tv mara tu baada ya kuitwaa kwa mara nyingine tena tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop wa Mwaka.

Ni katika kuenzi kazi za wakongwe katika burudani usiku wa 'red kapeti' Wasanii maarufu Diamond (mbele), Ali Kiba (shoto) na Banana Zorro (kulia) wakiimba wimbo 'Wanaume tumeumbwa mateso' wa Msondo nakuutia nakshi ambazo kwa kila aliye na jicho alisema naaam!
Usiku huu hakika ulikuwa mzuri sana kwa bidada huyu mdogo aliye na sauti ya kumtoa nyoka pangoni, LINAH alinyakuwa tuzo mbili: Msanii mpya anayechipukia na Mwimbaji Bora wa kike.

Ben Paul alitoka kidedea Wimbo bora wa RnB - Nikikupata.

Pichani Shabiki mteule wa Lady Jaydee akipokea tuzo kwa niaba yake ikiwa ni katika tuzo ya Msanii bora wa kike then tuzo ya pili wimbo bora wa Afrika Mashariki akishirikishwa na Kidumu.

Best Rapper of The Year (Band) Khalid Chokoraa na maswahiba wake Mapacha watatu.

Kaseja akimtunukisha Mzee Yusuph tuzo ya Wimbo bora wa taarab - My Valentine.

Mie na President wa Tanzania House of Talents ambaye vilevile ni mmoja wa wakuu wa bodi ya Clouds Media Group Mr Ruge Mutahaba.

'Shika ushikapo' toka kwao Mapacha watatu ft Mzee Yusuph ni wimbo ulionyakuwa tuzo ya Wimbo bora wa kiswahili.

Much Respect Kutoka kushoto: Bonta, J moo, G.sengo, Joe Makini na Niki wa Pili.