ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 18, 2011

MCHANGO WA MAAFA KUTOKA MWANZA 7,7,3

Sadiki Fadhili toka chuo cha SAUTI Mwanza akiwa na mkewe Husna Nasoro wakikabidhi msaada wao kwa Bonge wa Clouds fm, kuwaendea waathirika wa mabomu Gongo la mboto.

HIZI BANGI...

Kamanda Simon Sirro -Kutokana na juhudi za wananchi kushiriki kulisaidia jeshi la polisi kufichua waalifu nalo jeshi la polisi kuongeza nguvu katika misako yake kupitia oparesheni mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2010 – 2011 mkoani mwanza Jeshi hilo limefanikiwa kukamata madawa ya kulevya aina ya bangi kiasi cha kilo elfu moja mia tano sabini na tano na gramu 4.96.

Hayo yamebainishwa leo na Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa mwanza Simon Sirro wakati alipozungumza na waandishi wa habari mbele ya ofisi zake huku akionyesha baadhi ya vidhibitisho hivyo vya madawa mbalimbali ya kulevya yaliyokamatwa na jeshi lake.

Hili begi lilifungwa kama la msafiri ambalo unaweza dhani kuwa lina nguo lakini humo ndani liliku na robota la bangi iliyoshindiliwa kiuhakika.

Misokoyo na mitenba ya bangi iliyonaswa.
Madawa mengine yaliyokamatwa ni pamoja na mirungi kilo 3,769.106, Gongo lita elfu 10,638, na Noti bandia zenye thamani ya shilingi milioni sita laki saba tisini na tano elfu.

Kutoka TBC1 Richard Leo akiripoti....Kupitia misako mbalimbali kwa mwaka 2010 hilo limefanikiwa kukamata gramu mia mbili na kumi za madawa ya kulevya aina ya Cocaine na kiasi cha gramu mia sita hamsini na tatu za madawa ya kulevya aina ya Heroine.

KUPITIA 15599 SAIDIA GONGO LA MBOTO KWA HALI NA MALI

ANDIKA NENO maafa KISHA TUMA KWENDA NAMBA 15599Mkurugenzi wa mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba pamoja na meneja wa mfuko huo Yassaya Mwakifulefule wakishusha na kukabidhi vyakula mbalimbali wafanyakazi wa Red Cross waliopo katika kiwanja cha Uhuru kwa ajili ya kutoa huduma.

Picha hii ilipigwa kwa mbali asubuhi iliyofuata baada ya mlipuko wa mabomu, inaonyesha moshi ukifuka katika maghala hayo ya silaha eneo la gongo la mboto.

Baadhi ya watoto waliopotezana na wazazi au walezi wao wakiwa wamepewa hifadhi katika uwanja wa Uhuru.

Hapa kulikuwa na biashara ya duka na fundi cherehani.

Endapo usafiri ikatokea ukapatikana na kutokana na mahitaji kuwa makubwa zaidi ya uwezo wa vyombo vyenyewe vya usafiri, basi matumizi yalikuwa kama hivi pichani, muhimu kukimbilia sehemu iliyo salama.

Mabaki ya mabomu yaliyolipuka yakiwa yamekusanywa katika mojawapo ya vitongoji yalikoanguka.

Nyumba hii ilibomoka kutokana na vishindo vya mabomu.

Ili kusaidia ndugu zetu hawa walio katika kipindi kigumu nenda katika ukurasa wa sms (ujumbe mfupi), andika neno MAAFA kisha tuma kwenda 15599 ujumbe huu utakugharimu kiasi cha shilingi 1,000/= tu changia zaidi. Kupitia Vodacom. Na kwa wewe uliyepo Mwanza mkabidhi mchango wako BONGE wa Power Breakfast ndani ya Starmax Hotel iliyopo Kirumba.

@joseph nyaki.

NAHODHA WA AC MILAN GATTUSO AOMBA RADHI.

Nahodha wa AC Milan Gennaro Gattuso ameomba radhi kwa kumpiga kichwa kocha wa Tottenham Joe Jordan, baada ya timu yake kulazwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa timu 16 kuwania ubingwa wa Ulaya. Nahodha huyo wa AC Milaa mwenye umri wa miaka 33 ambaye siku za nyuma aliwahi kuichezea klabu ya Rangers ya Scotland, alizozana na Jordan mwenye umri wa miaka 59 na baadae akamsukuma kichwani. Sasa anasubiri kuadhibiwa kutokana na vitendo vyake vya utovu wa alivyoonesha uwanjani.

Awali alizozana na mshambuliaji wa Spurs, Peter Crouch na baadae akaoneshwa kadi ya manjano itakayomfanya asicheze mchezo wa marudiano, baada ya kumchezea rafu Steven Pienaar.

Mwisho wa mchezo, Gattuso alivua fulana yake na haraka akaelekea kumkabili Jordan, akimtolea maneno makali kabla ya kumpiga kichwa. Gattuso aliondolewa na wachezaji wenzake na akaacha ukali wake na kukumbatiana na mlinzi wa Spurs William Gallas.

Thursday, February 17, 2011

HALI NGUMU YAWAKABIRI WAKAZI WA GONGO LA MBOTO.

Pichani ni moja ya kipande cha mabomu yaliyolipuka katika kambi ya jeshi la wananchi Gongo la mboto jana usiku, taarifa zinasema kuwa vipande hivi vimezagaa katika maeneo mbalimbali baada ya milipuko ya jana iliyoleta maafa ya vifo vya idadi ya watu isiyojulikana, uharibifu wa makazi ya watu na rasilimali zao.

Misururu mikubwa ya watu imeonekana ikihama kutoka maeneo ambayo jeshi limeagiza waondoke kuepuka uwezekano wa milipuko mingine kutokea.

Nikipande cha bomu Tabata Chang'ombe.

Hali bado si shwari huko Gongo la Mboto kwani bado idadi kubwa ya watoto na wakazi wa maeneo hayo wanaendelea kupelekwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Wananchi wameombwa kushiriki kwa hali na mali kuwawezesha kwa chakula, kuwasitiri kwa nguo na kwa njia yeyote wakazi hao.

HILL WAY BAND - KIZAZI KIPYA ROCK CITY.

Sasa wakazi wa kanda ya ziwa wamepata tiba ya kiu ya burudani kwa ujio wa bendi mpya inayoitwa 'HILL WAY' ni bendi inayoundwa na vijana waliobobea katika mafunzo ya muziki sambamba na uzoefu kwa kupiga katika bendi mbalimbali hapa nchini na Kongo. Mpiga gitaa la besi Abineli akionesha ujuzi wake mbele ya kamera ya Clouds tv.

Ni ndani ya kipindi kifupi tu takribani miezi 3, bendi hii imewakamata wapenzi wa muziki wa dansi Mwanza na kuziba pengo la wakazi wa mji huu kukosa burudani ya muziki wa dansi wa kisasa levo za Akudo, Fm, Twanga na kadhalika.

Bendi hii yenye vijana waliona hamu ya mapinduzi katika tasnia ya burudani inamwaga raha katika viunga vya Hill way pub, MJ pub na kushughulika na mialiko mbalimbali.

IJUMAA HII WANAPIGA PALE MJ PUB KONA YA BWIRU NENDA UKAWAONE!
SOON NTAKULETEA KIKOSI KAMILI.

7,7,3 WAVAMIA SOKO LA SAMAKI LA ILOGANZALA .

Jana wadau wa Leo tena, Kwa raha zetu na Club 10 walipata fursa ya kutembelea soko maarufu la samaki Iloganzala lililopo wilayani Ilemela jijini Mwanza na kujionea shughuli mbalimbali za biashara hiyo muhimu kwa uchumi wa watu waishio mkoani hapa.Wajaluo wanakauli 'Kamongo tamu sinda nyama' Chunguza mjomba utabaini!

Wadau wa Clouds jicho kwa jicho na matayarisho ya kamongo.

Ikiwa ni ahadi ya leo tena kukutana na BACHELA WA MWANZA kumpikia na kumpa 'full sevisi' za jikoni na haya ndo maandalizi yenyewe! Dina akinunua mboga MABACHELA MUPOOooooo!!

Gea Habib akitoa zawadi ya pasi kutoka ZEC.

Gea akitoa zawadi toka wadau wa Vifaa vya umeme ZEC ambao ni moja ya wadhamini wa 7,7,3 Mwanza.(miaka 7leo tena, 7kwaraha zetu na 3club kumi).

Wachuuzi wa samaki aina ya nembe.

Zamaradi akilisha ndege mwarabu wake.

Wapara samaki si kuparua magamba pekee hata kukutayarishia minofu, kinachobaki baada ya minofu kutolewa ndiyo chaitwa MAPANKI.

Dereva namba moja wa safari za 7,7,3 Mwanza, Paul Stone akiwa amebeba samaki aina ya kamongo.

BREAKINGNEWS MABOMU YALIPUKA TENA DAR SAFARI HII GONGO LA MBOTO

HABARI TULIZO ZIPATA USIKU HUU ZINASEMA MABOMU YAMELIPUKA TENA JIJINI DAR ENEO LA GONGO LA MBOTO. TAHARUKI IMEZUKA KUTUATIA MILIPUKO MIKUBWA YA MABOMU ILIYOTOKEA GHALA LA KUTUNZIA SILAHA LA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ), GONGOLAMOTO, HUKU KUKIWA NA TAARIFA ZA WATU KUFA NA ZAIDI YA 100 KUJERUHIWA. Mmoja wa walionusurika kwenye tukio la kuangukiwa na ukuta, Juma Nganyanga, alisema kuna uwezekano ya maiti wengine kuwa chini ya ukuta huo.

Nganyanga alisema aliona kundi la watu wakiwa wamekimbilia kupumzika kwenye baraza la nyumba hiyo baada ya kukimbia nyumba zao, wakati wakiwa katika maombi ya kuomba Mungu awaepueshe na janga hilo, ghafla aliona vumbi likitimka kwenye nyumba hiyo.

Mwenye nyumba hiyo, Farida Magwa, ambaye alikuwa akibubujikwa na machozi alisema akiwa barabarani na familia yake, aliambiwa kuwa nyumba yake imepigwa bomu na kuna watu wameuawa. Alisema baadaye waliweza kutoa maiti za watu watano, wakiwamo watoto wawili, lakini kuna uwezekano wa wengine bado wapo wamefunikwa na kifusi cha ukuta huo.

Habari zaidi zinasema mamia ya wananchi wameyakimbia makazi yao. Mamia ya watu kutoka Gongolamboto, Karakata, Tabata, Segerea, Ukonga, Kitunda, Banana na maeneo mengine jirani, wameonekana wakipanda daladala, wengine wakining'inia nyuma ya magari hayo yaliyokuwa yakielekea katikati ya jiji, huku mamia kwa mamia ya watu walikuwa wakitembea kwa miguu kuokoa maisha yao.

Ni hii mara ya pili kwa milipuko kama hiyo kutoka jijini Dar es Saalam katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, mwaka wa 2009 zaidi ya watu ishirini waliuawa na wengine 300 kujerihiwa.


kwa picha zaidi tenbelea MICHUZI.

Wednesday, February 16, 2011

UCHAGUZI MKUU UGANDA KUFANYIKA IJUMAA.

Wagombea wa kiti cha urais na ubunge nchini Uganda, wanatarajiwa kukamilisha kampeini zao hii leo tayari kwa uchaguzi mkuu utakaofanmyika siku ya Ijumaa.Rais Yoweri Museveni, ambaye anawania muhula wa nne kama rais wa Uganda, kupitia chama tawala cha national Resistance Movement, NRM, anatarajiwa kufanya kikao na waandishi wa habari leo asubuhi, kabla ya kukamilisha kampeini yake na mkutano wa hadhara mjini Kampala.


Nae Mpinzani mkuu wa rais Museveni, Kizza Besigye (pichani kushoto) anayewania kiti hicho kupitia chama cha Forum for Democratic Change, FDC, naye atakuwa na mkutano katika chuo kikuu kimoja mjini Kampala.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, Badru Kiggundu, ametoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya kisiasa nchini humo, kuvunja makundi yote ya wapiganaji ambayo yaliundwa kwa dhamira ya kulinda masanduki ya kupigia kura.

Blogu hii ya jamii inawatakia Uchaguzi Mwema wa Amani wananchi wa Uganda.

HEKA HEKA ZA MWANZA NA GEA HABIB.

Mamaa wa heka heka Gea Habib kazini eneo la kona ya Bwiru : sakata la madreva wa pikipiki kuchoma gari mara baada ya mwenzao kugongwa na gari na kufariki dunia. Kwa muda wa wiki nzima Vipindi vya leo tena, kwaraha zetu na club 10 vinaendelea kusikika LIVE toka 88.1 Mwanza na kusikika kote nchini.

Huyu ndiye Gea mwenyewe.

Meneja wa Vipindi Clouds Radio Sebastian Maganga akitoa maelezo kwa mtangazaji wa Leo tena 'muvi leo' na Take One ya Clouds Tv, hapa ni juu kabisa ya jengo la NSSF Mwanza, juu ya ghorofa ya tisa eneo la Swimming pool.

Mtaa wa Uhuru eneo la Delux.

Walipotembelea Zai Fashion and Botique, Kutoka kushoto ni Mtayarishaji wa leo tena Moonshine, Sebastian Maganga, Mamaa Zai wa Zai Fashion, Zamaradi Mketema na Dina Marious.

DUH!.....SOKOMOKO..

Nilikuta watu wamejaa vutanikuvute ikiendelea, Huyu jamaa alipita njia isiyoruhusiwa (one way) huku aking'ang'ania kwenye usukani, mara baada ya kukamatwa aligoma kushuka toka kwenye gari alilokuwa akiendesha.

Mara wakamchomoa toka kwenye uskani... alikuwa akikimbizwa na polisi toka mbali na polisi hao walisikika wakisema "umetusumbua kweli sasa tumekunasa".

Shaka-shaka pia imejitokeza kwamba gari alilokuwa akiendesha jamaa huyu lasemekana kuwa ni la wizi.

Tuesday, February 15, 2011

7,7,3 YA LEO TENA, KWARAHA ZETU, CLUB 10 NA CLOUDS FM WATAMBULISHWA KATIKATI YA USIKU WA VALENTINE MWANZA.

Hapa ni katika kujuana zaidi usiku wa Valentine Nyumbani Hotels Mwanza, aliyeshika kipaza ni Meneja wa Clouds Radio Sebastian Maganga, MD wa Humajo Entertainment Edith Cesilia Subet, Gea Habib, Dina Marious, Zamaradi Mketema, na PG. Kweka.

Barnaba na Linah wa Mwanza wakikamua wrong number.

Da place....

Askwambie mtu Rangi zilipangwa zikapangika Mwanawane... kinginez' Cheki Samaki wanavyo pendezesha flowers wa Mwanza.

Mkali toka THT unaye mkubali Amini ambaye alikuwa ni mmoja wa mabrazaz waliosababisha utamu kunoga katika sekta ya burudani Valentine 2011 mwanza.

Mc G.Sengo na 'supa staa Amini'

Kila kitu kilikuwa supa bin supari - lazima ucheze..

Ingawa Lady walitinga Red nao men kutupia kitu cha white... haikujalisha wenye Colour nyingine ruksa Ha-Ha-Ha!

Maua ya kuvutia, yenye kunukia yalikuwa mengi ileee..... Ni NOWMA yaaaaani Haina Majjotro'.

'Best Couple' Mr.George Masha na my Wifewake mara baada ya kutunukiwa zawadi zao.

Shukurani za dhati kwa wakazi wa Mwanza kwani shughuli ni watu na watu ndo sisi. Salamu za upendo wa dhati toka kwaaaa.. Othman Michuzi pichani ambaye nae alikwea pipa kujumuika nasi siku ya wapendanao.

Kwa Wiki hii nzima Clouds fm 88.1 Mwanza itaendelea kurusha kipindi cha Leo tena LIVE na kusikika kote Nchini hadi siku ya ijumaa, hivyo ewe mkazi wa Mwanza endelea kutoa ushirikiano kwa Radio yako.