ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 2, 2011

VODACOM YATUA RASMI MWANDOYA, WANANCHI WASEMA NI ZAIDI YA MAWASILIANO

Mara baada ya blogu hii sambamba na kituo cha Clouds Fm, Chanel Ten pamoja na magazeti mbalimbali nchini kuripoti juu ya kadhia inayosababishwa na mawasiliano duni wanayoipata wananchi vijiji vya Mwandoya makao makuu ya jimbo la Kisesa wilayani Meatu, ikisababisha wananchi hao kutafutana shati kwa shati, wakilazimika kusafiri umbali wa kilometa kadhaa kusaka huduma za utumaji na upokeaji fedha au zile za kibenki.

Mtandao wa simu za mkononi Vodacom tayari umekwisha tinga eneo hilo, hivyo kuanzia sasa wananchi wake wanawasiliana bila tabu na ndugu na jamaa zao toka meneo mbalimbali nchini na hata nje ya nchi.
Yu mmoja wa wananchi wa Mwandoya wanaoamini kuwa Vodacom inapotua mahali ni zaidi ya mawasiliano kwani inauwezo wa kutatua hata suala lao la kibenki. Kupitia huduma ya M-PESA, wanapokuwa mbali itarahisisha suala la kuwatumia pesa za matumizi wazazi, ada ya shule kwa wanafunzi hata kuhifadhi pesa zao mara baada ya mauzo kwa zao lao kuu la pamba, nao wafanyabiashara kuagiza bidhaa mijini hasa ukizingatia kuwa hakuna benki iliyojitokeza kutoa huduma kijijini hapo watapata fursa kuagiza mizigo na kutuma fedha pasina kusafiri.

Katibu wa CCM wilaya ya Maswa Omary Kalolo (kushoto) naye alikuwepo katika eneo la tukio kutoa sapoti kwa tukio zima la uzinduzi wa mawasiliano ya Vodacom lililofanywa na Mh. Luhaga Mpina Mbunge wa jimbo la Kisesa wilaya ya Meatu (mwenye suti nyeusi katika).

Moja ya changamoto zinazoikabili wilaya ya meatu ni upatikanaji wa nishati ya umeme.

Hata hivyo zaidi ya bilioni 1.6 zimetengwa kupitia bajeti ya serikali kuipatia umeme wilaya ya Meatu na vijiji vyake ambapo mpaka sasa miundombinu ya nguzo imekwisha simikwa huku mradi ukitegemewa kukamilika rasmi mwezi desemba 2011 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete anategemewa kuzindua mradi huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.