ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 15, 2011

MKUU WA MKOA WA MWANZA ERENEST NDIKILO ATINGA OFISI ZA WANDISHI WA HABARI MWANZA, AHAIDI KUUNDA TUME KUFUATILIA MAUAJI YA MWANDISHI RICHARD MASATU

Mkuu wa mkoa wa Mwanza bwana Erenest Ndikilo ofisi yake imeahidi kuunda kamati ya kuchunguza kifo cha utata cha mwandishi wa habari kanda ya ziwa marehemu Richard Masatu aliyefariki dunia mnamo tarehe 10/08/2011 nakupatikana na tundu la jeraha lililoanzia chini ya kidevu hadi kwenye koromeo.

Hayo ameyasema leo kupitia ombi lililo ambatanishwa kwenye risala yao alipotembelea Ofisi za chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mwanza (MPC) kwa lengo la kuzungumza nao.

Mkuu huyo wa mkoa amewaasa wandishi waepuke kutumiwa na baadhi ya wanasiasa kuchafua wenzao kwa kuandika habari zinazo poteza amani, utulivu, mshikamano na wala wasitumike kuigawa nchi kikabila, kidini na kisiasa badala yake watumie taaluma zao kushauri, kukosoa, kutoa mapendekezo na kusifu pale viongozi wanapotenda stahiki kwa jamii.

Aidha Mh. Ndikilo amewaagiza wakuu wote wa halmashauri zote za wilaya mkoani Mwanza kutoa ushirikiano kwa wanahabari ili wananchi wapate taarifa zilizo sahihi na kwa wakati.

Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Wandishi wa Habari Mwanza (MPC) bi Flora Magabe akiwasilisha Risala kwa mh. mkuu wa mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo(kushoto) na aliyesimama katikati ni katibu wa MPC Edwin Soko.

Mwisho mkuu wa mkoa amewasihi wandishi wa habari kuwa na utaratibu wa kufika sehemu za vijijini kukusanya habari , taarifa na matukio kwa lengo la kuikwamua jamii hiyo muhimu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.