ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 17, 2011

KUSHEREKEA MIAKA 40 YA KONYAGI KAMPUNI YA TDL YATOA MISAADA YA VIFAA VYA USAFI KWA JIJI LA MWANZA.

Mike Mrema ambaye ni Meneja wa Mauzo na Usambazaji kanda ya Ziwa toka kampuni ya TANZANIA DISTILLERIES LIMITED (TDL) akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa kaimu mkurugenzi wa jiji la Mwanza Fransis Mkabenga(left) ili viwasilishwe kwa makundi mbalimbali yaliyosajiliwa na ofisi za jiji hilo.

Kwa upande wake Afisa afya wa jiji mazingira na usafi bw. Dontora Kamenya ameishukuru kampuni ya Konyagi kwa msaada huo kwani uhaba wa vifaa na vitendea kazi imekuwa changamoto kuu inayovikabili vikundi vingi vya kufanya usafi vilivyo chini ya Halmashauri ya jiji hivyo ofisi yake imeahidi kuvipa uangalizi mzuri.

Nia ya msaada huo ni kuchangia juhudi za kuimarisha usafi katika majiji ya Mwanza, Arusha na Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kuchangia maendeleo ya jamii ambapo TDL imeahidi kuhamasisha kampeni za usafi wa mazingira katika kuendeleza usafi na maandari safi ya majiji.

Sekta ya habari waalikwa Mr. Deus (Tanzania Daima), Abdalah Tilata (Star Tv), Sheila Sezzy (Mwananchi), John Maduhu (Mtanzania) na Grace Chilongola (Habari Leo).

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Matoroli 20, Vest zenye reflectors 50, Gloves 50, Marsk 50, Kofia za usalama 50, Miwani ya kuzuia vumbi na jua 50, Gum boots 50, Mifagio 50, Jembe 50 na Reki 50 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni kumi.

Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mwanza Fransis Mkabengwa ametoa wito kwa wafanyausafi wa jiji kuvitumia kwa uangalifu vifaa hivyo bila kuvifuja ili vitumike kwa muda mrefu katika suala la kutunza mazingira.

Wito pia umetolewa kwa mashirika mengine kuiga mfano huo wa TANZANIA DISTILLERIES LIMITED kuunga mkono juhudi za serikali kwenye harakati mbalimbali za kuihudumia jamii hasa suala la usafi na utunzaji wa mazingira.

Pamoja na msaada huu Konyagi imeahidi kwa siku za baadaye kutoa mapipa makubwa ya kuhifadhia taka.

Katibu wa Usafi Wafagizi jiji la Mwanza bi Fatma Ramadhani- "Tatizo la kutapisha vyoo hasa kwa watu waishio milimani ni sugu, tunakutana na taka za vinyesi, nyingine za siri hazija hifadhiwa kiusalama, wafanya usafi wamekuwa wakikumbwa na magonjwa mengi hivyo nawaomba maafisa afya, wenyeviti wa vitongoji kuhamasisha jamii nyumba hadi nyumba kuchimba vyoo vya kudumu"

Kwa kauli moja Jumuiya ya wafanya usafi jijini Mwanza imeimba jamii kuithamini na kuiheshimu kazi hiyo muhimu katika suala zima la utunzaji wa mazingira kwani bila ya kufanya usafi sote tutaangamia kwa magonjwa.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Abdallah Tilata naona yuko makini na kamera ya Sengo! Big up bwana

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.