ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 1, 2011

MPINA::KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA KUJENGWA MAKAO MAKUU YA JIMBO LA KISESA.


Mbunge wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu Mh.Luhaga Joelson Mpina (CCM) mwishoni mwa wiki amefanya mkutano wa hadhara kijiji cha Mwandoya ambako ndiko makao makuu ya Jimbo, lengo kuu likiwa kuainisha na kubainisha mikakati ya maendeleo iliyopo na inayotarajiwa kufanyika jimboni humo.

Kwa mujibu wa Mpina Tayari jimbo la Kisesa limepata mwekezaji wa kujenga kiwanda cha kuchambua pamba ambacho ujenzi wake utaanza rasmi pindi umeme utakapoingia Mwandoya mnamo mwezi desemba mwaka huu.

Faida zinazotajwa kupatikana pindi kiwanda hicho kitakapojengwa na kuanza kufanya kazi ni pamoja na vijana wa jimbo la Kisesa kupata ajira, wakulima watapata fursa ya kuuza pamba yao kwa bei nzuri zaidi kwani wanunuzi wengi hupunguza bei ya zao hilo kwa kisingizio cha gharama za usafirishaji kwenda kwenye vinu vya kuchambua pamba.

Burudani nayo haikukauka hapa ni kwaya ya Mwandoya ikitumbuiza.

Raha ilipozidi kiongozi wa kundi aliimba begani mwa mwananchi.

Kijiji hiki cha Mwandoya kinaonekana kukuwa kwa kasi katika suala zima la maendeleo kutokana na juhudi za dhati za mbunge Joelson Mpina sambamba na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wananchi wa jimbo lake kwani ndani ya kipindi cha miaka miwili kupitia changizi mbalimbali tayari wamefanikiwa kujenga Zahanati moja pamoja na nyumba nane za walimu wa shule zinazozunguka eneo hilo.

Wazee wa wakimsikiliza mbunge wao.

Kwa lengo la kukuza vipaji vya soka Mh. Joelson Mpina, alikabidhi jezi seti moja moja kwa timu za Mwandoya Shooting na Maskani Football Club.

Kakaaaa nawe upo-po hapa....!!!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.