ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 24, 2011

WANAOSITA KUJIVUA GAMBA FAGIO LAJA KIKAO KIJACHO CCM, WATENDAJI WABOVU SERIKALINI LAO PIA LAJA.

CHUNGULIA KIDEO:Ni sehemu ya majibu kupitia maswali aliyoulizwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Mnauye wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika ziara yake aliyoifanya hivi majuzi jijini Mwanza.
“Ni suala la maadili na ujumla wake, maadili yanapimwa na nini? Maadili yanapimwa na imani ya Chama Cha mapinduzi, ukiapa kule nyuma unasema ‘Rushwa ni adui wa haki sitapokea wala kutoa rushwa, Cheo ni dhamana sito tumia cheo changu wala cha mwingine..’ Kwa hiyo siyo suala la Nape wala la nani, hili ni suala la Chama, Nape atakufa yatabaki haya"

"Yamekuwepo mimi sijazaliwa, nimezaliwa nimeyakuta, nitayasimamia nitaondoka nitayaacha……”

“Sasa tukimaliza huku tutaelekeza nguvu zetu Serikalini ambako nako kuna watu ambao hawafanyi sawa…..”

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.