ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 23, 2011

MAN U' YAZABWA 6-1 UWANJA WA NYUMBANI.

Kinyume na matarajio ya Wengi, Man United walishindwa kabisa kuhimili vishindo vya majirani zao na mahasimu wao wa jadi. Hadi mapumziko City walikuwa wakiongoza kwa goli moja lililofungwa na Mario Balotelli.

Man United walicheza karibu kipindi chote cha pili wakiwa na mchezaji mmoja pungufu baada ya beki Jonny Evans kupewa kadi nyekundu kwa kumzuia Balotelli kwenda kumuona kipa wa United David De Gea.

Baada ya kutolewa kwa Evans, karamu ya magoli ilianza kwa City. Balotelli aliongeza bao la pili katika dakika ya 60. Sergio Aguero akafunga bao la tatu katika dakika ya 69. Edin Dzeko baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba alifunga bao la nne katika dakika ya 90, David Silva bao la tano na Dzeko tena kupiga msumari wa mwisho katika filimbi ya mwisho ya mchezo.

Bao pekee la kufutia machozi la United lilifungwa na Darren Fletcher katika dakika ya 81.

Matokeo haya yanaipa City pointi tatu ambazo zinaifanya kuendelea kuongoza kwa pointi tano zaidi ya United.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.