ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 23, 2011

MADA MAUGO KUIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA LEO CCM KIRUMBA MWANZA

Mada Maugo (kushoto) na Joseph Odhiambo wakitambiana.
BONDIA Machachari nchini Mada Maugo amesema kuwa atamchapa kipigo cha mbwa mwitu bondia mwenzake kutoka nchini Kenya, Joseph Odhiambo kwenye shindano la raundi nane la ngumi linalotarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba kesho(leo).

Aliyasema hayo jana muda mfupi mara baada ya kufanyika zoezi la kupimwa uzito kwa mabondia wote 12 watakaoshiriki katika pambano la leo.


Mada Maugo.
Huku akionekana kujiamini akitumia kauli yake ya uzawa, Maugo alisema kuwa yuko bomba na amewataka watanzania na wapenzi wa ngumi hususani wale wa Kanda ya ziwa wajitokeze leo kwa wingi kuupata uhondo na kushuhudia jinsi ambavyo anamshikisha adabu jirani yake bondia kutoka nchini Kenya Joseph Odhiambo.

Maugo v/s Odhiambo
Naye Joseph Odhiambo kutoka nchini Kenya, licha ya kukiri kumfahamu Mada Maugo katika ulimwengu wa masumbwi na kuwashukuru wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa, alisema kuwa hana hofu juu ya pambano hilo kwa madai kuwa ametoka mbali na anaamini atashinda katika pambano hilo la raundi 8 kwa uzito wa kilo 72 (middle weight).

Joseph Marwa.
Jumla ya mabondia 12 watashiriki, ambapo pambano la utangulizi litakuwa ni kati ya mabondia maarufu nchini Rashid Matumla ambaye atacheza na Bondia kutoka mkoani Mara Emma Kichele katika uzito wa kg 79 light weight na Joseph Marwa atafungua dimba na bondia Irandi Chacha naye kutoka Musoma katika uzito wa kg 83 cruiser weight.

Kiingilio katika pambano hilo kitakuwa ni Sh. 5,000 jukwaa kuu, Sh. 3,000 mzunguko na Sh. 1,000 kwa watoto.


Mabondia wengine watakaoshiriki na uzito wao kwenye mabano ni Elias Amos(56kg) VS Said Mazola(55kg), Pande Yusuph(55kg) vs Gabriel Paulo(56kg), Gasto Rweyunga(60kg) vs Deo Msangi(59), Ibrahim Wegoro(59) vs Nassor Ally(60kg). Mabondia wengine wanaotarajiwa kusindikiza pambano hilo ni pamoja na Frank Jofrey(64kg) vs Alex Nyakalungu(63kg) na Saliboko Juma(66kg) vs Danny William(68kg).

Katika pambano hilo, wasanii wa kizazi kipya John Walker, Ras Lion na D nob wanatarajiwa kuwatumbuiza wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa na wapenzi wa mchezo kutoka mikoa jirani ya kanda ya ziwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.