ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 19, 2011

DAKTARI MTANZANIA JULIE MAKANI APOKEA TUZO KUTOKA ROYAL SOCIETY PFIZER LONDON

Dr Julie Makani Akipokea Tuzo yake.

Wageni waalikwa kwenye Royal Society Pfizer Awards London

Dr Julie Makani. akiwa na Cleo, Paul na Frank baada ya kupokea Tuzo.

Parliamentary Under Secretary of State, International Development Stephen O'Brien. akimpongeza Dr Julie Makani PG

Dr Julie Makani akiwa na familia yake

Kutoka Kulia Balozi Kallaghe, Mama Makani, Dr Makani, MP O'Brien, Naibu Balozi Chabaka na Mr Simba

Dr Julie Makani kutoka Tanzania amepokea Tuzo jumanne tarehe 18 octoba 2011 ya Royal Society Pfizer nchini Uingereza. Dr Makani amepokea tuzo hii ya utafiti alioufanya katika gonjwa hatari la Sickle Cell (SCD) ambaye makazi yake ya kazi ni kwenye Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi cha Muhimbili katika idara ya Haematology. Kutokana na utafiti wake kumeonekana ushahidi kuwa, chanzo kukuu cha magonjwa na vifo vitokanavyo na sickle Cell nchini Tanzania husababishwa na Arnemia (upungufu wa damu)

Dr Makani pia amefanya mchakato wa matibabu katika majaribio ya Hydroxyure chemotherapy agent inayo gusa Bone marrow katika matibabu ya Anaemia kwenye ugonjwa Sickle Cell

Ni matumaini yake kuwa utafiti huu utapelekea kuboresha uchunguzi na matibabu ya ugonjwa huu ili kuweza kuimarisha afya za watu, mfumo mzima wa afya na jamii kwa ujumla.
Kwa niaba ya Watanzania wote blogu ya G. Sengo inatoa pongezi kwa DR Makani kwa mafanikio hayo.


Asanteni.
Urban Pulse.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.