ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 18, 2011

MASHITAKA 8 KATI YA 9 'TUPA KULE' KESI YA KUPINGA MATOKEO ILEMELA, KESI YAHAIRISHWA WALALAMIKAJI WAINGIA MITINI

Wakili Tundu Lisu akitoa maelezo ya mwenendo wa kesi hiyo huku mteja wake Mbunge Highness Samson (wapili kuia) akimsikiliza kwa makini.
Kesi namba 12/2010 yakupinga matokeo ya uchaguzi mkuu jimbo la ilemela mkoani Mwanza iliyompatia ushindi mbunge kupitia tiketi ya CHADEMA bw. Highness Samson imeahirishwa tena leo jioni katika mahakama ya rufaa jijini humo.

Wakili T. Lisu (kulia) akiwa ameambatana na mteja wake mbunge H. Samson wakitoka kwenye ukumbi wa mahakama.
Kati ya mashitaka tisa yaliyofunguliwa dhidi ya mbunge wa sasa wa Ilemela mashitaka nane yametupiliwa mbali na kubaki shitaka moja tu ambalo ni dai la watu wapatao laki moja na elfu kumi na nne kudaiwa kuzuiwa kupiga kura.

Shitaka hilo lililosalia linaonekana kukosa nguvu kwani linafananishwa na kesi ya uchaguzi ya mwaka 1995 ya bw. Silvester Masinde na Pius Msekwa, ambapo Mahakama ya Rufaa Tanzania iliamuru kuwa kura ambazo hazikupigwa au hazikuhesabiwa kugawanywa kwa uwiano wa asilimia walizopata wagombea kwenye uchaguzi.

Mashitaka nane yaliyofutwa ni pamoja na kufanyika kampeni kwenye vituo vya kupigia kura na makanisani siku ya kupiga kura, wafuasi wa chadema kuzuia watu wasipige kura, mgombea wa chadema na mawakala wake kutoa rushwa kwa kujenga visima kwa wapiga kura na kutoa vinywaji na vyakula kwenye misiba, mahela yalitolewa kwenye eneo la Manguruwe, mshtakiwa mbunge pamoja na mawakala wake walinunua shahada za wapiga kura, kulikuwa na mabadiliko ya vituo vya wapigia kura vituo vya soko la Kirumba na kwenye viwanja vya Furahisha, jingine ni kuwa kuna mawakala wa Sangabuye na Buhongwa hawakula kiapo cha kutunza siri.

Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza Jack Fish' akiteta jambo na mh. mbunge na wakili wake mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo ambapo inategemewa kusomwa tena Ijumaa hii 21oct2011.

Matokeo ya uchaguzi huo yanayopingwa ni kuwa Highness Samson aliweza kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Ilemela kwa kumshinda Anthony Diallo wa CCM kwa kura 31,269 dhidi ya kura 26,270 hii ikiwa ni tofauti ya kura 4,999.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.