ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 22, 2011

MSONDO YATWAA TUZO ya the Best Rhumba Group katika East Africa Music

BENDI ya muziki wa dansi nchini Msondo ngoma imepata TUZO ya the Best Rhumba Group katika East Africa Music Awards mashindano yaliyofanyika Nairobi Kenya na kukusanyika kwa bendi za Afrika Mashariki na bendi ya msondo kuibuka Kidedea katika mashindano hayo akithibitisha ushindi huo meneja wa bendi Saidi Kibiriti alipokuwa akiongea na Msemaji wa Bendi hiyo, Rajabu Mhamila , Super D Alisema wameshinda tuzo hiyo na watahakikisha wanaionesha kwa mashabiki wa bendi hiyo ili kudhirisha kuwa bendi hiyo ipo ngangari popote duniani mana bendi imekamilika kila idara alisema Super D (pichani)

Bendi hiyo itanza mazoezi siku ya jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na sikukuu ya Iddi inayotarajia kufanyika wiki ijayo ambapo wanaingia kambini kusuka vibao vipya ikiwemo na kuvifanyia kazi vile vya Zamani

Super D alisema bendi hiyo siku ya Iddi Mosi itapiga katika viwanja vya TTC Chang'ombe ambapo mashabiki watapata kuona tuzo hiyo ya Afrika Mashariki walioitwaa hivi karibuni na kupata fulsa ya kupiga nayo picha katika viwanja hivyo

Bendi hiyo inayotamba na vibao vyake vipya vya Suluu utunzi wake Shabani Dede na Nadhili ya Mapenzi uliotungwa na Juma Katundu


Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
Mob;+255787 406930
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.