ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 21, 2011

MA-MISS LAKE ZONE NA LUNCH YAO MELINI LEO

Ndiyo hawa hapa.. Je ni nani kuchomoka na taji? Jibu jumamosi hii tr23....!


Second ofisa wa meli ya Victoria Godifrey Kalikayo akitoa maelezo kwa washiriki wa miss lake zone walipotembelea meli hiyo kujionea utendaji kazi.

Hii ndiyo dira kionyesha uelekeo kwa waongoza meli.

Mv Victoria ni meli yenye uwezo wa kubeba mzigo wa tani 200 na abiria 1200 inafanya safari zake ndani ya ziwa victoria kutoka Mwanza hadi Bukoba mkoani Kagera.

Baada ya kuzunguka na kuishuhudia jiografia melini humo warembo hao walipata fursa ya kupata chakula cha mchana.

Hizi ni safari za mwisho mwisho kwa warembo hao kuelekea siku ya jumamosi tupate kushuhudia kinyang'anyiro cha kumsaka Mnyange wa Miss lake Zone atakaye jumuika na washiriki wenzake toka kundini kwenye Miss Tanzania baadaye mwaka huu.

Je ni katika kundi hili....?

Wapishi sanjari na wahudumu wa hoteli ya melini humo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.