ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 19, 2011

UKATILI GANI HUU? MWANAMKE AKATWA KIGANJA CHA MKONO AKATWA MAGOTI YOTE MAWILI NA MUMEWE.

Mwanamke mmoja mkazi wa Nyabiroga Songa Bunchari Bi. Agnes Chacha (25) amefyekwa kiganja chake cha mkono pamoja na magoti ya miguu yote miwili na mume wake na kukatika vibaya tukio likitokea jana usiku ambapo kwa hivi sasa amelazwa katika wod 6 hosptali ya wilaya ya Tarime akipata matibabu.

Akizungumza kwa uchungu na kulia kwa maumivu makali ya majera Bi Agnes amesema kuwa juzi majira ya saa mbili mume wake aitwaye Chacha Hamis alimkata kigaja chake na kutoroka kusiko julikana mara baada ya mwananke huyo kuchelewa kurejea nyumbani.

Bi. Agnes amesema kuwa alifika nyumbani hapo saa mbili usiku akitokea kwenye biashara yao ya duka ambayo iko katika senta kijijini hapo na alichelewa kwa sababu juzi ilikuwa ni siku ya soko hivyo wateja huwa wengi ambapo mara nyingi huwa wanachelewa hata wakati mwingine wakiwa na mume wake.

Agnes akihojiwa na Helena Magabe mwandishi wa Habari hii .
Akiendelea kuzungumza kwa majonzi ya maumivu makali amesema kuwa baada ya kufika nyumbani aliwaagiza watoto wake kumfatia unga wa muhogo kwa wifi yake ambapo watoto walimwambia kwamba wanaogopa kwani ulikuwa usiku hivyo akalazimika kubandika maji jikoni na kwenda mwenyewe.

Baada ya kutoka kwa wifi yake akiwa na unga wake alimkuta mume wake akiwa amekaa nje na panga lake mkononi ambapo alimwuliza sababu za yeye kufikia nje akiwa na panga na kuongeza kuwa mume wake alimwuliza kuwa alikuwa wapi naye akajieleza vizuri.

“ mimi nina mamba ya mwezi mmoja imenisababishia kuuchukia ugari wa mahindi ndio maana linifata mwenyewe licha ya kwamba ulikuwa usiku lakini mume wangu hakutaka kunisikiliza japo nilikuwa na unga akaanza
kunilazimisha niseme nilikuwa wapi na na nilikuwa na nani” alisema.

Akiendelea kusimulia amesema mumewe huyo aliendelea kumlazimisha kusema aliyekuwa naye ndipo atamsamehe naye bila hiyana mwanamke huyo akaamua kumtaja bwana Muhiri kijana ambaye mume huyo amekuwa akimlazimisha kuwa ni mpenzi wake baada ya kupata maneno ya watu.

Akifafanua amesema kuwa mume wake huyo aliwahi kufungwa kipindi cha vita ya koo na aliporudi uraiani watu walimwambia kwamba mke wake Bi Agnes alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Muriri hivyo mume wake tangu hapo akamwekea kinyongo jamaa huyo ingawa anadai walikuwa wanakiiishi vizuri.

Miguu.
Amesema kuwa baada ya watoto wake kuona amekatwa kiganja na kiganja hicho kuruka mbali walipiga yowe hivyo watu wakakusanyika ambapo baada ya kuwa amepata fahamu alimkuta shemeji yake, wifi yake pamoja na mke mwenzake wakifanya jitihada za kupata gari kwajiri ya kumpeleka hosptali.

Licha ya Bi.Agnes kufanyiwa ulemavu wa maisha amesema kuwa akipona atarudi kwa mume wake kwa sababu akiolewa mke mwingine atanyanyasa watoto na kuongeza kuwa hawezi kupokelewa na mtu mwingine akiwa na mkono mmoja ikiwa ni pamoja na kukosa ajira yoyote akiwa katika hali hiyo.

Muuguzi wa zamu ambaye hakupenda kutajwa jina lake amesema waliokuwepo katika zamu usiku waligoma kumtibu wakitaka barua toka polisi ambapo na jana asubuhi baada ya kuona wauguzi wamembana sana
kusema ukweli alisimulia kisa kizima ambapo polisi walifika wodini hapo na kumchukuwa maelezo.

“ wifi yake alikuwa hapa alikuwa anaficha sana na ana mdomo sana lakini na sisi tukajua ni mume wake amemkata na kweli ni mume yaani matukio kama haya ni mengi sana hapa hivi ulkuwaga wapi jamani kufatilia watu wamekatwa mikono, miguu, hata wengine wawili walikuwa hapa ungewahi kidogo tu ungewakuta” alisema muuguzi huyo.

Baadhi ya wanawake walio kumbwa na sekeseke kama hili ni pamoja na Nyangi Wansama Ryoba mkazi wa Nyamongo (31) aliyekatwa mgongo na mume wake ambaye ameruhusiwa kuondoka jana na mwingine ni Deborah Lucas Jockson(38) mkazi wa Buhemba wilayani Trime ambaye amepigwa na kuumizwa vibaya maeneo ya nyonga na mbavu zake kiasi cha kutembelea upande mmoja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.