ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 20, 2011

AIRTEL YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 50 SHULE YA SEKONDARI KANGAYE

Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi leo imegawa msaada wa madawati kwa shule ya sekondari Kangaye jijini Mwanza ikiwa ni sehemu zake za kuisaidia jamii. Pichani meneja wa masoko kanda ya ziwa Ally Maswanya akikabidhi mchango huo kwa uongozi wa Shule.

Meneja wa shughuli za kijamii Tunu Kavishe amesema kuwa Airtel mara baada ya kuona uhaba uliopo kwa shule nyingi nchini ili kuisaidia serikali kampuni yake imedhamiria kutoa zaidi vifaa mbalimbali vya elimu na kufundishia kama sehemu yake muhimu katika kuikwamua jamii.

Mstahiki meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata hiyo ya Nyakato bw. Josephat Manyerere: Ameishukuru sana Airtel kwa kuichagua Mwanza kama sehemu moja wapo ya kuinua elimu na amefurahishwa kusikia kuwa mpango huo kuwa ni endelevu kwani utapunguza uhaba wa madawati na nyezo za elimu kwa mashule.

Wanafunzi wa shule ya Kayange wawakilishi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na madawati yao.

Sehemu tu ya wanafunzi walio hudhuria hafla hiyo ya makabidhiano.

Airtel mkombozi wa jamii, Airtel mkombozi wa Elimu nchini Airtel Oyee!

Meneja wa shughuli za kijamii Airtel Tunu Kavishe akishiriki zoezi la kuingiza madawati madarasani.

Ni miaka saba sasa tangu Airtel ilipoanza mpango wake wa kusaidia nyenzo mbalimbali za elimu ikiwemo vitabu kwa shule za sekondari hapa nchini ambapo hadi sasa shule takribani 800 zimenufaika na mpango huo.


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania Jackon Mbando akielekeza njia iendayo shule ya Sekondari Kangaye iliyoko kata ya Nyakato wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.