ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 27, 2011

AIRTEL RISING STAR MWANZA YAANZA RASMI LEO

Michuano ya Airtel Rising star kwa mkoa wa Mwanza imeanza rasmi leo viwanja vinavyotumika ni uwanja wa Buswelu Sekondari, Michuno ikifunguliwa nae mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi hapa akiikagua timu ya Taqwa Sekondari.


Mgeni rasmi akikikagua kikosi cha Buswelu Sekondari.

Katika mchezo huo wa pili Taqwa waliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Buswelu (pichani).


"Mcheze mpira mzuri, uliojaa ushindani pamoja na ufundi mkiwa na nidhamu ndani yake, kumbukeni kuwa siyo wote mtaenda ngazi ya taifa bali ni vijana sita hivyo itumieni vyema nafasi hii kuiwakilisha Mwanza na sehemu yake ya ajira kwa zama zijazo. Kila mmoja acheze akiweka nadhiri moyoni mwake kuwa MIMI LAZIMA NIWE KATI YA WALE SITA" @Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro.

Kwenye mchezo wa awali leo nayo Nsumba Sekondari imeibamiza timu yenye majigambo mengi vijana wa mjini Mwanza Sekondari 1-0


Taqwa Sekondari ( red) wakipeleka mashambulizi langoni mwa Buswelu Sekondari hekaheka zilizozaa bao la ushindi.

Ni soka na NIDHAMU yake.

Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano hayo mkoa wa Mwanza Job Mushumba amesema kuwa michezo ya ligi hiyo katika hatua inayofuata itachezwa kwa njia ya mtoano yaani Fist looser kucheza na Second looser kupata mshindi wa tatu na First winner kucheza na Second winner kumpata bingwa wa kituo cha Mwanza,

Michezo yote hiyo inataraji kuchezwa jumamosi ya wiki hii kiwanja nitakwambia papahapa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.