ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 28, 2011

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI KUPITIA BIA YA BALIMI EXTRA LAGER-KAGERA.

Mgeni Rasmi Mh. Ndyamukama Katibu Tawala (W) Bukoba akihutubia Mashindano ya Ngoma za Asili yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Balimi Extra lager, kushoto ni Andrew Mbwambo Meneja Mauzo na Erick Mwayela, Meneja Matukio kanda ya ziwa.

Mshindi wa kwanza Mashindano ya Ngoma za Asili kundi la Rugowoile kutoka manispaa ya Bukoba akishapokea fedha taslim laki tano(500,000/=) kutoka kwa mgeni rasmi Mh. Ndyamukama, hapa anasalimiana na Andrew Mbwambo Meneja Mauzo Kampuni ya Bia. Mshindi wa pili ni Rugu toka Karagwe walijipatia laki Nne(400,000/=), wa tatu ni Kabale toka Manispaa ya Bukoba walijipatia laki tatu(300,000/=).

Kundi la Rugowoile kutoka manispaa ya Bukoba wakishangilia mara baada ya kutangazwa washindi wa kwanza.

Kundi la Rumanyika kutoka Karagwe wakionyesha umahiri wao wa ngoma za asili.

Haya ndio mambo yalivyokua katika viwanja vya Kaitaba katika kumsaka mshindi wa mashindano ya ngoma za asili kupitia kinywaji cha Balimi Extra lager.

Makundi mbalimbali yakionyesha umahiri wao.

Shughuli bado inaendelea ...

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.