ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 28, 2011

WAYDAD USO KWA USO NA SIMBA LEO MISRI.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Misri kuchezesha pambano la mkondo mmoja kati ya Simba ya Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco litakalofanyika LEO Mei 28 2011 Uwanja wa Petrosport jijini Cairo, Misri.Simba Sc mazoezini.

Mechi hiyo ya kutafuta timu ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya MabingwaAfrika itaanza saa 12 kamili jioni kwa saa za Cairo. Waamuzi hao ni Farouk Mohamed atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Mohamed Waleed na Hassan Sherif. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni OmarFahim wakati Kamishna wa mchezo huo ni Magdy Shams El Din kutoka Sudan.

Wydad Casablanca.

Mshindi wa mchezo wa leo atacheza kundi B pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, Esperance ya Tunisia na Moloudia Club d’Alger ya Algeria.

Timu itakayoshindwa itaingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo itacheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni 10, 11 na 12 mwaka huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.