ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 3, 2011

KUTOKA KWA KAMANDA SIRRO LEO.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Simon Sirro.

ACHOMWA KISU KISA WIVU WA MAPENZI
Mnamo Tarehe 1/5/2011 majira ya saa moja usiku huko katika kijiji cha Buhama kata ya Nyakasasa wilayani Sengerema, mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Deus Kasimu (25) amepoteza maisha mara baada ya kuchomwa kisu kwenye bega la kushoto na mtu aliyetambulika kwa jina la Maulid Mustapha.

Kisa cha tukio hilo kinatajwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Mtuhumiwa alikimbia mara baada ya kufanya uhalifu huo.


OPARESHENI WAUAJI.
Nacho kikosi cha Udhibiti mauaji yanayo shirikisha imani za ushirikina kilichoundwa hivi karibuni kanda ya ziwa na kuanza rasmi kazi siku ya jana ya tarehe 2/5/2011 kinaendelea kufanya kazi zake na majibu ya oparesheni hiyo yasema kuwa tayari watu zaidi ya 25 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani mwanza kwa mahojiano.

Wilaya zinazohusishwa na Oparesheni hiyo ni pamoja na Sengerema, Geita na Misungwi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.