ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 28, 2011

KINA CHA MAJI ZIWA VICTORIA KIMEPUNGUA MITA 2.57 : WARSHA YA WADAU WA MAZINGIRA KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI ILIYOFANYIKA MWANZA YABAINISHA

Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Mwanza Bi. Clesencia Joseph.
Mabadiliko ya Tabia nchi ndilo sasa tatizo linaloleta changamoto kubwa sana duniani hasa katika ukuaji wa uchumi, ustawi wa jamii na maendeleo endelevu kwa bara la Afrika.

Madhara yanazidi kuwa makubwa hasa kwa nchi changa na zenye uchumi unaotegemea hali ya hewa kama kilimo na uzalishaji wa umeme. Ambapo takribani asilimia 34 ya ardhi bara la Afrika ko katika hatari ya kugeuka jangwa.

Watu milioni 200 hawapati chakula cha kutosha ;
Asilimia 75 ya watoto wanaokufa kwa maralia inatokana na uchafuzi wa maralia;



Ripoti ya nne ya jopo la wana sayansi wanaofanya utafiti kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (The Intergovernmental Panel on Climate-IPCC) iliyotolewa mwishoni mwa mwaka 2007 imeonyesha kuwa joto la dunia limeongezaka kwa wastani wa 0.74 sentigredi tangu mapinduzi ya viwanda.

Wadau wakibadilishana mawazo.
Kwa upande wa Tanzania tayari athari zimeanza kujitokeza, kina cha maji Ziwa Victoria kimepungua kwa mita 2.57, Ziwa Rukwa limepungua kwa kilomita 7 kwa kipindi cha takribani miaka 50 iliyopita. Kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari baadhi ya visima vya maji safi katika mwambao wa Pwani ya Bagamoyo na Pangani sasa vimeingiliwa na maji ya chumvi na vingine havitumiki kabisa hivyo kuathili upatikanaji wa maji safi na salama.

Nchi yetu pia inashuhudia kuenea zaidi kwa ugonjwa wa maralia katika maeneo ambayo haukuwa kawaida kama maeneo ya mkoa wa Kagera, Mbeya, Lushoto na Amani mkoani Tanga.

Picha ya pamoja ya Wanawarsha Mazingira.
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, inaendelea kuelimisha umma na wataalamu katika sekta na taasisis za umma pamoja na sekta binafsi kuhusiana na tatizo la mabadiliko ya Tabianchi na kujiandaa vyema kukabiliana na tatizo kwa ujumla.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.