ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 27, 2011

SHUSHO, BONY MWAITEGE, ROSE MUHANDO, UPENDO NKONE, ANASTAZIA MKABWA, GELARDIN ODUOR, SOLOMON MUKUBWA WATIKISA MWANZA TAMASHA LA PASAKA.

Hicho kiatu....... watu walivua kweli kujumuika nae mwimbaji wa muziki wa injili Anastazia mukabwa.

Upendo Nkone akiruka kwa afya zake ndani ya utumishi tamasha la Pasaka Mwanza uwanja wa CCM Kirumba chini ya waandaaji Msama Promotion.

Hakika Mungu ni mwaminifu na wema wake, fadhili zake ni za milee ni maneno ndani ya wimbo usiochuja uitwao 'Mungu ni mwaminifu' wake Solomon Mukubwa toka nchini Kenya..

Christina Shusho akimwaga mibaraka kwa watu wa Mwanza..

Kwa Mungu kuna raha bhanna! ilipendeza sana na kuvutia wengi pale mwimbaji wa muziki wa injili Christina Shushoa alipo mwita Rose Muhando kucheza nae wimbo Ndoa, akichagiza zaidi watu kupendana ndani tamasha la aina yake la msimu wa pasaka jijini Mwanza lililoandaliwa na Msama Promotion..

Mwimbaji wa muziki wa Injili toka nchini Kenya Geraldin Oduor akiimba kwa hisia na pembeni akipewa sapoti na Christina Shusho (kushoto)..

Bonny Mwaitege akimkumbatia mmoja kati ya waimbaji mtoto mara baada ya kuimba kwa uzuri katika tamasha la pasaka CCM Kirumba..

Ni vijana wa Revival Mission Band wakiwa katika engo yao kama mashuhuda mara tu baada ya kuhudumu..

Nyuma ya sound walisimama rafiki hawa kutoka kushoto ni Samadu Abdul, Mzee wa Hossana blog na braza kutpka Kwaneema Fm Mwanza..

Hapa jee!.

Wanadada hawa walipendeza na magauni yao mazuri walichagua pahala hapa pa utulivu kushuhudia yanayojiri ndani ya Tamasha la pasaka lililoandaliwa na Msama Promotion..

Vijana anglican nyamanoro wakihudumu zao mbili kali.

Philadelphia kwaya kutoka Mwanza.

Shalom band.

Raha ya muziki wa injili hapa ilikuwa ni Rose Muhando jukwaani..

Ni jambo lisilofichika kwamba muziki wainjili unaraha yake bwana, mama huyu alinyanyuka kwenda kucheza na kijana huyu kudhihirisha kwamba raha aliyonayo..
\
Cameraaaaa... almuradi kila mmoja anataka kubaki na kumbukumbu yake nyumbani kwake..

Bonny mwaitege na rafiki zake watoto..

Watu wanajua kushine bwana chekshia hapa.

Tupe maoni yako

3 comments:

  1. sengo ungetuwekea player tusikiliza hizo kwaya

    ReplyDelete
  2. hillo rose muhando you so good song may god bless you very much

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.