ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 8, 2011

MASANJA WA ZE ORIJINO KOMEDI KUWA MC, NAYE 20% KUMWAGA BURUDANI MISS KILIMANJARO 2011

Shindano la kumsaka mnyange wa Kilimanjaro 2011 linategemewa kuanza hivi karibuni baada ya waandaji wa shindano hilo kudai kuwa sehemu kubwa ya maandalizi imeanza kukamilika ikiwa na pamoja kuwakusanya warembo kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya mazoezi (catwalk).

Msemaji wa shindano hilo Bw.Methuselah Magese amesema kuwa yeye na mundaji mkuu wa shindano hilo Jaquekline Chuwa tayari wako katika mchakato mnene kuhakikisha miss Tanzania wa mwaka huu anatokea mkoani Kilimanjaro.

Shindano la miss Kilimanjaro litafanyika june 11 juni katika hoteli nya Salsanero iliyoko Shant town mjini Moshi ambapo mchekeshaji masanja toka kundi la Ze Komedi Orijino atakuwa ndiye mc wa siku hiyo wakati msanii 20% na wengine wengi wataburudisha vya kutosha.

Miss kilimanjaro 2011 imedhaminiwa na Vodacom, Redds, Africa sana pub,Rafiki min super market, Excutive solution, Bamm solution na www.uniqueentertz.blogspot.com.

"Tunawaomba warembo wanaojiamini kuwa wao ni warembo na wenye ari ya kuwa vinara wa sanaa ya urembo wajitokeze kuwania taji hilo ambalo litakuwa na ushabiki wa aina yake kwani tunategemea kutoa warembo bomba ambao watatoa changamoto kwa vitongoji na kanda zingine" alisema magese.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.