ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 26, 2011

* MCHAMBUZI ANDY GRAY ATIMULIWA Sky.

Kampuni ya Sky imemtimua mara moja mchambuzi na mtangazaji wa soka Andy Gray.GRAY and KEYS.
Mchambuzi huyo ambaye tayari ameshapewa adhabu kwa matamshi yake yaliyolenga ubaguzi wa kijinsia dhidi ya mwamuzi mwanamke Sian Massey, kabla ya mchezo wa siku ya Jumamosi kati ya Wolves na Liverpool. Gray mwenye umri wa miaka 55 pamoja na mwenzake Richard Keys, waliondolewa kuchambua mechi ya Jumatatu kati ya Bolton na Chelsea. Na siku ya Jumanne, Sky walisema wanakatisha mkataba wa Gray kutokana na ushahidi mpya "usiokubalika wa matamshi ya utovu wa nidhamu."

Taarifa iliyotolewa na kampuni ya Sky imeendelea kueleza: "Ushahidi mpya, unaohusu matamshi yaliyotolewa kwenye televisheni mwezi wa Desemba mwaka 2010, yameunganishwa baada ya Andy Gray tayari kupewa adhabu ya utovu wa nidhamu kutokana na matamshi yake aliyoyatoa tarehe 22 mwezi wa Januari, 2011."

Mkurugenzi mtendaji wa Sky Sports, Barney Francis amesema: "Mkataba wa Andy Gray umesimamishwa kutokana na tabia yake isiyokubalika. Baada ya kutolewa onyo siku ya Jumatatu, tumeona hakuna haja ya kusubiri kuchukua hatua zaidi baada ya kupata taarifa mpya." Wakati huo huo Massey, ameondolewa kuwa msaidizi wa mwamuzi katika mechi ya siku ya Jumanne ya ligi daraja la pili kati ya Crewe na Bradford.


Tukio zima lilianza siku ya Jumamosi, wakati Keys na Gray, walipoamini vipaza sauti vyao vimezimwa, na wakanukuliwa wakisema mwamuzi huyo Massey na waamuzi wasaidizi wengine wanawake, "hawafahamu sheria ya kuotea". Keys alimpigia simu Massey, ambaye alikubali kuombwa radhi na mtangazaji huyo.

Hata hivyo picha nyingie iliyoneshwa katika televeshini, siku ya Jumatatu ambapo Gray alizungumza na mwandishi wa Sky Sports, Andy Burton kuhusiana na Massey.

Sky iliripoti watu hao wawili walikuwa wakizungumzia kuhusu mwamuzi Massey muonekano wake, huku Burton akimwita Massey "ni mrembo anayevutia" wakati Gray akihoji: "Wanawake wanafahamu nini juu ya sheria ya kuotea?"

Mapema siku ya Jumanne, ilitangazwa Burton "alizungumza na kuonywa" kuhusiana na matamshi yake na sasa hatahusishwa katika matangazo ya mpambano wa nusu fainali ya Kombe la Carling siku ya Jumatano, kati ya Birmingham na West Ham.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.