ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 9, 2010

DUME CUP IMEANZA KUSHIKA KASI KWA KIPIGO KIKALI.

BAADA YA KUZINDULIWA MICHUANO YA LIGI SOKA YA
(DUME CUP) MKOANI MWANZA TIMU KUMI NA SITA ZA MADEREVA NA WAPIGA DEBE ZA VIJANA WENYE UMRI WA MIAKA KUMI NA TANO HADI AROBAINI NA TANO ZIMEANZA KUJIHAMI KUTWAA UBINGWA WA LIGI HIYO.


KATIKA MCHEZO WA UFUNGUZI AMBAO UMEFANYIKA KWENYE UWANJA WA MABATINI, KIKOSI CHA TIMU YA SOKA YA MASKANI FRESH KIMEFANIKIWA KUTOA DOZI YA KICHAPO CHA MABAO 5 KWA 4 DHIDI YA KIKOSI CHA TIMU YA SOKA YA MWANZA COMPLEX.

LENGO LA LIGI HIYO NI KUWAELIMISHA VIJANA KUHUSU NAMNA NA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI. BAADA YA MICHUANO HIYO KUZINDULIWA MADEREVA NA WAPIGA DEBE MKOANI HAPA WATABADILIKA NA KUCHUKUA TAHADHARI YA NAMNA YA KUEPUKA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKANA NA ELIMU INAYOKWENDA SAMBAMBA NA MICHUANO HIYO.

ZAWADI KWA MSHINDI WA KWANZA NI NG’OMBE DUME NA KOMBE, WA PILI NI KOMBE NA MBUZI, WA TATU NI KOMBE PEKEE HUKU WASHIRIKI WALIOSALIA KUPATA ZAWADI MBALIMBALI ZA KIFUTA JASHO ZIKIWEMO TISHETI ZENYE UJUMBE HUSIKA KAMA SHUKRANI YA USHIRIKI.

Friday, October 8, 2010

KUNANI KULEee!

NI UKARIMU AU?
ARAMBA- ARAMBA- AAaaM! AAAaaM!!

NA PIAAAAaa! NADEKEZWA MIE NAPAKATWA.

MTANGAZAJI WA REDIO MIRAYA ILIYOPO SUDAN KUSINI Bi. Lubna Lasu akiwa mzigoni...safii take 5 DADA AKEE!

WANANCHI WA KABILA LA DALINGA LILILOPO SUDAN KUSINI WAKIGOMBANIA CHAKULA KILICHOPELEKWA HAPO NA UMOJA WA MATAIFA KUPITIA MPANGO WAKE WA WFP. KIDOLE NA MACHO TUSIUMIZANE...

HAFLA FUPI YA RAIS KIKWETE KUSHEHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA USIKU WA KUAMKIA LEO.

Rais Jakaya Kikwete akimlisha keki mkewe Mama Salma Kikwete usiku wa kuamkia leo,Mh Jk usiku wa kuamkia leo alikuwa anatimiza miaka 60.

Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Prof Jay pamoja na Mwana FA wakizungumza jambo na Rais Kikwete na pia kumpa pongezi za dhati kabisa kwenye hafla hiyo iliyokuwa ya kuvutia usiku wa kuamkia leo.

Rais Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd,Juhayna Ajmi.Rais Kikwete alipita kila meza kusalimiana na wageni waalikwa waliofikwa kwenye hafla yake fupi ya kusherehekea kuzaliwa kwake usiku wa kuamkia leo.

KUWA SEHEMU YA WAHUDHURIAJI TEMBELEA www.michuzijr.blogspot.com

Thursday, October 7, 2010

AKUDO KUITIKISA MWANZA JUMAPILI YA WIKI HII.

NI JUMAPILI HII UKUMBI VIJANA SOCIAL KIRUMBA MWANZA.

KAMPENI ZA UCHAGUZI 2010 VIUNGA VYA MWANZA CUF WABISHA HODI MLANGONI MWAKO.

NI KATIKA KAMPENI ZA CUF NYUMBA KWA NYUMBA, MTAA KWA MTAA, PICHANI MSEMAJI MAHIRI TOKA CUF BW. SHIDO AKIMNADI DAUDI SULEIMAN MKAMA ANAYE GOMBEA UDIWANI KATA YA MBUGANI.

SERA ZINAMWAGWA NA KAMPENI ZINAENDELEA KWA AMANI NA USALAMA MTAA WA UHURU.

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU KITUO CHA MWANZA.


MH. MKUU WA MKOA WA MWANZA ABBAS KANDORO AKITOA HOTUBA YA UFUNGUZI WA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAK 30 YA TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU KITUO CHA MWANZA TRH 7 OCT 2010.
MH ALIONA MENGI YENYE KUSTAHILI SIFA NA AKASEMA NI JAMBO LA KUJIVUNIA KUONA KUWA TANGU KUANZISHWA KWA KITUO HIKI KIMEWEZA KUFANYA TAFITI MBALIMBALI ZINAZOJULIKANA KIMATAIFA AMBAZO PIA ZIMETOA MCHANGO MKUBWA KTK KUIMARISHA SERA.


MOJA WAPO YA UTAFITI WA KIMATAIFA NA KUWEZESHA MATOKEO YAKE KUTUMIKA KUTENGENEZA SERA NI ULE ULIOBAINI KUWA UKIDHIBITI MAGONJWA YA KUJAMIIANA UNAPUNGUZA KASI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA 40%. UTAFITI ULIOFANYIKA MWANZA .KUANZIA 1991 HADI 1994 NA KUHUSISHA WASHIRIKI WAPATAO 12,000.

KAIMU MKURUGENZI NIMR MWELE MALECELA AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI NA ALIYEKETI PAMBENI YAKE NI MKUU WA KITUO CHA UTAFITI MWANZA.

MEZA KUU.
KITENGO HIKI CHA UTAFITI KIMEAHIDI KUTOA MATOKEO KWA LUGHA YA KUELEWEKA ILI WANANCHI WOTE WAJUE KILICHOFANYIKA KWA KIPINDI CHOTE CHA UTAFITI CHA MIAKA 30 NA YALE YATAKAYO JIRI KTK TAFITI ZINAZOKUJA.

JENGO LA NIMR MWANZA.
MOJA KATI YA TAFITI TATU AMBAZO ZIMEWEZA KUORESHA SERA NA HUDUMA NI ILE YA TIBA NA DALILI KWA AJILI YA MAGONJWA YA ZINAA AMBAPO UTAFITI UMEONYESHA KUWA TOHARA KWA WANAUME INAVYOWEZA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI NA HATIMAYE KITENGO KUSABISHA UANZISHWAJI WA SERA MPANGO WA KUFANYA TOHARA NCHI NZIMA.

KITUO CHA NIMR MWANZA KUPITIA UTAFITI WAKE KIMEWEZESHA MATIBABU YA UGONJWA WA KASWENDE KWA AKINA MAMA WAJAWAZITO, UGONJWA ULIOKUWA UKIWALETEA MATATIZO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO, UTAFITI HUO TAYARI UMEONYESHA KWAMBA VIPIMO VYA PAPO HAPO VILIVYOTENGENEZWA MIAKA YA HIVI KARIBUNI VINAFAA NA MGONJWA ANAWEZA KUPATA MAJIBU SIKU HIYO NA KUANZA MATIBABU TOFATI NA SIKU ZA NYUMA AMBAPO MGONJWA ALILAZIMIKA KUSUBIRI KWA SIKU ZAIDI YA MBILI KABLA YA KUPATIWA MAJIBU.

AMEWASIHI WATAFITI HAO WA NIMR KITUO CHA MWANZA KUTOBWETEKA NA MAFANIKIO WALIYOYAPATA BALI KUENDELEA KUCHAPA KAZI KWA BIDII ILI KULILETEA HESHIMA TAIFA HILI.

MKUU WA MKOA WA MWANZA KATIKA STORI ZAKE ALIZUNGUMZIA ILE TABIA YA KUPENDA CHIPS MAYAI KWA SANA AU PILAU UNAKAMUA MAFUTA YANACHURUZIKA MKONONI HADI KWAPANI TUNAFURAHIA AKASIHI TUACHANE NAYO. TULE CHAKULA BORA, TUZINGATIE KANUNI ZA AFYA TUFANYE MAZOEZI NA KUHAKIKISHA KUWA TUNAISHI KTK MAZINGIRA MASAFI.

WASHIRIKI WA UFUNGUZI WA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU KITUO CHA MWANZA.

KATIKA MAADHIMISHO HAYO VYETI VYA KUTAMBUA HUDUMA WALIYOIFANYA KUTUMIKIA TAASISI YA UGONJWA WA MATENDE VILITOLEWA. PICHANI NI ELIZABETH BUGUMBA AKIPOKEA CHETI CHAKE TOKA KWA MGENI RASMI.

JAMAA MASHUHURI SANA WILAYA YA UKEREWE DR. MASHAURI.

ANTHONY SITENGA WA KITENGO CHA KARAKANA AKIPOKEA CHETI CHAKE.

KAIMU MKURUGENZI NIMR MWELE MALACELA AMESEMA KUWA OPEN DAY ZITAFANYIKA KATIKA MAENEO YA VIWANJA VYA NIMR NA HIVYO ANAWAKARIBISHA WANANCHI WOTE WALIO JIJINI MWANZA KUFIKA NA KUONA KAZI ZA TAFITI ZIFANYWAZO.

KILELE CHA MAADHIMISHO HAYO KITAKUWA TRH 20 0CT 2010 AMBAPO MAONESHO NA HAFLA VITAFANYIKA MAKAO MAKUU DAR ES SALAAM.

HAPPY BIRTHDAY RAIS WA TANZANIA MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE.

Jakaya Mrisho Kikwete (born October 7, 1950) is a Tanzanian politician, the fourth and current President of the United Republic of Tanzania. Kikwete was born in Msoga, Bagamoyo District, Tanganyika in present day Tanzania.

UPENDO KWA WATU WAKO HI HULKA YAKO.
BLOGU HII YA JAMII (gsengo) INAKUTAKIA KILA LA KHERI RAIS JK KATIKA HARAKATI ZAKO NJEMA.

Wednesday, October 6, 2010

MWANZA, SHINYANGA JIANDAE NA DUME CUP.

SHIRIKA LINALO JISHUGHULISHA NA UTOAJI WA BIDHA ZA KIAFYA NA KUHAMASISHA ELIMU YA MAHUSIANO MEMA, AFYA YA UZAZI MAMA NA MTOTO T-MARC KWA KUSHIRIKIANA NA DUME CONDOM LIMEANDAA LIGI YA MTOANO KWA MASHINDANO YA MCHEZO WA SOKA INAYOKWENDA KWA JINA LA DUME CUP.
MRATIBU WA MASHINDANO HAYO GERLARD NDIMILA AMESEMA MASHINDANO HAYO YATAHUSISHA WILAYA 4 AMBAPO MBILI NI KUTOKA MKOA WA MWANZA NA MBILI KUTOKA MKOA WA SHINYANGA, MKOA WA MWANZA NI WILAYA YA NYAMAGANA NA GEITA NAKO SHINYANGA NI WILAYA ZA KAHAMA NA SHY TOWN.
MASHINDANO HAYO YA MTOANO YA DUME CUP YATAKAYO FANYIKA KATIKA WILAYA HIZO TAJWA YAMELENGA KUZISHIRIKISHA TIMU ZA WAVUVI, WAFANYAKAZI WA MIGODI, WAUZA MITUMBA, MAGAZETI, WAPIGADEBE NA WASUKUMAJI MIKOKOTENI.

NAYE MJUMBE WA KAMATI YA CHAMA CHA SOKA MKOANI MWANZA (MZFA) MUTANI YANGWE AMEONGEZA KWA KUSEMA KUWA MASHINDANO HAYO YANAYOTARAJI KUANZA KUSHIKA KASI KUANZIA TAREHE 8,OCTOBER 2010 YATAENDESHWA KWA KUTUMIA SHERIA NA KANUNI ZA SOKA ULIMWENGUNI FIFA NA KUSIMAMIWA NA WAAMUZI WENYE VIWANGO WANAO TAMBULIWA NA TFF.
SAMBAMBA NA VIKOMBE KWA MSHINDI WA KWANZA NA WAPILI ZAWADI NYINGINE KWA KWA MSHINDI WA KWANZA NI DUME LA NG’OMBE NA MBUZI WAWILI HUKU MSHINDI WA PILI AKIKAMATA KIKOMBE NA MBUZI MMOJA HUKU WASHIRIKI WALIOSALIA KUZAWADIWA T-SHIRT ZILIZOBEBA UJUMBE WA KUHAMASISHA MCHAKATO MZIMA.

SHIRIKA LA T-MARC KUPITIA DUME CUP PAMOJA NA KUTUMIA MASHINDANO HAYO KUCHUNGUZA NA KUFANYA TATHMINI YA JUU YA ELIMU ITOTOLEWAYO KAMA INAFIKA IPASAVYO VILEVILE SHIRIKA HILO LITATUMIA NAFASI HIYO KUTOA TENA NA TENA ELIMU YA MATUMIZI YA CONDOM IKIWA NI MCHANGO WAKE KWA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA VIRUSI VYA UKIMWI.
UDHAMINI WA DUME KATIKA MASHINDANO HAYO (DUME CUP) UMELENGA MAENEO YENYE MAAMBUKIZI MAKUBWA YA VIRUSI VYA UKIMWI, SEHEMU ZA BIASHARA, BIASHARA YA USAFIRI, KILIMO CHA BIASHARA, MACHIMBO YA MADINI NA BIASHARA YA UVUVI.

TAMASHA LA EARTH DANCE LILIVYOFANA JIJINI MWANZA.

THE SUKUMA DANCE KUTOKA BUJORA MWANZA WAKITOA BURUDANI PALE TUNZA LODGE.

ZAIDI YA WATAZAMAJI 750 WALIHUDHURIA TAMASHA HILI JIJINI MWANZA LILILO MAHSUSI KUOMBA AMANI DUNIANI NA KUTANGAZA UTAMADUNI WA NCHI HUSIKA KWA MATAIFA MBALIMBALI.

CHURAaaa! SURA KWA MUGONGO.

KUNDI LA WARRIORS & FIREDANCERS TOKA ARUSHA LILIKAMUA REGGAE BALAaa!MUZIKI WAKE ULIZIA CARIBEAN BEAT.

DADA HUYU PAMOJA NA KUIMBA ALIKUWA AKIZIMUDU TUMBA ILE KIB- KIBINGWA.

FLOWERS NA FACE PAINTING YAKE HUKU AKIFURAHIA UTAMU.

PICHANI NI SUKUMA DANCERS TOKA BUJORA NA MING'AO.

KIKAZI ZAIDI NA MBLOGISHAJI WAKO WA MATAIFA YA MBEFELE.

MBALI NA BURUDANI YA MUZIKI NA NGOMA WATOTO WA MITAANI WALIPATA FURSA YA KUJIFUNZA MBINU KUHUSU UCHORAJI, MBIO ZA BOTI NA MASHINDANO YA KUCHEZA MUZIKI HUKU WATU WAKIJINUNULIA BIDHAA MBALIMBALI ZA ASILI.

TEHE THI-THI! MDAU ALIPOISTUKIA KAMERA YA BLOGU YAKO.

NYAMA, NYAMA, NYAMAA! JIBU - nyama!
YA NYOKA! JIBU - ......!


JAMAA ALIKAMATA BATA ZA KUTOSHA KISHA NYOKA AKAGEUKA KUWA TAI YA KUVAA SHINGONI. NDIPO NIKAPATA MBINU - KAMA WE U MWOGA, UKITAKA KUMSHIKA NYOKA, PIGA KITUNGI, MBONA UTAMTIA HADI KINYWANI.

BURUDANI ILIENDELEA HADI NITE KALI BABAKE KWA SHOW KALI TOKA KWA MWAMBA WA KASKAZINI JOE MAKINI.

FLOWERS IN ZA HOUSE!

MSANII MWINGINE WA HIP HOP ALIYEKAMUA USIKU HUO NI BABALUKU TOKA NCHINI UGANDA, KWA MASHABIKI MBONA SHANGWE!!


MISOSI MBALIMBALI ILIKUWEPO KUANZIA KUKU, SAMAKI CHOMA, HADI CHAKULA CHA KI-SOUTH CHAITWA 'POIKA' (INATAMKWA PWIKI) KILIKUWEPO. Aaaa! KWA FLOWERS HIZI, HATA KAMA UTAKUWA MBALI KIVIPI, USIKOSE TENA MWAKANI MWANA WANE!

JOE MAKINI NA (....) WAKE.